• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

ZIARA YA MADIWANI NA KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO KATIKA MIRADI

Posted on: October 22nd, 2022

Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba inayotekelezwa kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwemo Serikali kuu, halmashauri kupitia mapato ya ndani na kupitia nguvu za wananchi.

Kamati hii ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Projestus Tegamaisho na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Ndg. Tapita S. Tuvana waliongoza kamati katika ukaguzi wa Miradi ya maendeleo ya Ujenzi wa Mnada wa Kimataifa wa Nkelenge, Ujenzi wa Shule mpya ya sekondari Kitobo, Ukaamilishaji wa Maabara shule ya sekondari Bwabuki, Ujenzi wa Kituo Kipya cha Afya Kanyigo, Ujenzi wa Zahanati Mpya ya Buturage, Ujenzi wa Zahanati Mpya ya Kakiri, Ujenzi Zahanati mpya ya Nkerenge, Eneo la maegesho ya Malori Mutukula na Eneo la uwekezaji Mutukula.

Katika Mnada wa Kimataifa wa Nkerenge uliopo kata ya Mutukula katika kijiji cha Nkerenge ambao unajengwa na Wizara ya Mifugo kupitia mkandarasi aitwae PLANCON LIMITED na serikali imetoa shilingi milioni 395 kwa awamu ujenzi wa awamu ya kwanza unaojumuisha ujenzi wa uzio, mazizi manne, sehemu ya kupandishia na kushushia mifugo kwenye magari, sehemu ya kunyweshea mifugo na choo cha matundu 06 na ujenzi unaendele vizuri.

Zira ililenga katika kuona Halmashauri inaweza kuweka kitega uchumi gani katika mazingira yanayozunguka mnada ili kuweza kuongeza vyanzo vya mapato vya Halmasha pamoja na kuboresha mazingira kufuatia uwekezaji mkubwa ulioletwa na wizara ya mifugo.

Waheshimiwa Madiwani walisisitiza kwamba wanataka wafanya biashara watakao kuja katika kijiji hiki waweze kupata huduma zote za muhimu katika kijiji hiki na waweze kuwa fursa ya kiuchumi kutokana na kukutana kwa watu wa mataifa mbalimbali katika mnada huu.


Ujenzi wa shule Mpya ya Sekondari kitobo ambao unajumuisha Madarasa 8 na ofisi 04 za walimu, ujenzi wa maabara za Physics, Chemistry na Biology, ujenzi wa jengo la utawala, maktaba, ICT, ujenzi wa vyoo vya matundu 10 ya wavulana na matundu 10 wasichana na vyanzo vya fedha vya ujenzi huu ni SEQUIP milioni 470 na Mapato ya ndani shilingi Milioni 100.

Kamati ya fedha imempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Missenyi Bw. Waziri Kombo kwa kutoa fedha kwa wakati na kufanya usimamizi na ufuatiliaji mkubwa sana hadi ujenzi kufikia katika hali iliyopo hivi sasa bila kusimama na mpaka siku ya ziara mafundi wanaendelea na ujenzi.


Kaimu mkurugenzi kwaniaba ya Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anaboresha sekta ya elimu baada ya kutupatia shilingi milioni 90 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara ya Physics, Chemistry na Biology katika shule ya sekondari Bwabuki na mpaka kufikia siku ya leo ujenzi umekamilika kwa asilimia 100.


Kutokana na tozo za miamala ya simu Mhe. Mwenyekiti alimshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea shilingi Milioni 500 kwa awamu mbili kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kanyigo ambapo jengo la wagonjwa wa nje na maabara yamekamilika na sasa ujenzi unaendelea wa Kichomea taka,  wodi ya wazazi, jengo la upasuaji na jengo la kufulia.

Kamati iliwasihi wasimamizi wa ujenzi kuhakikisha taratibu zote za ujenzi zinafuatwa pamoja na utunzanzaji wa nyaraka za ujenzi huo.

Katika kuwasogezea wananchi huduma kkaribu, serikali kuu ilitoa nyakati tofauti shilingi milioni 50 kwa kila zahanati katika  zahanati ya Kakiri iliopo Kata Kakunyu, Zahanati ya Buturage iliopo kata Bugandika na Zahanati ya Nkerenge iliopo Kata ya Mutukula kwa kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hizo baada ya wananchi wa maeneo hayo kujenga mpaka hatua ya boma.

Aidha kupitia mapato ya ndani halmashauri ilitoa shilingi milioni 09 katika zahanati ya Kakiri na Imetenga shilingi milioni 10 kwa ajili ya Zahanati ya Nkerenge kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa miundo katika zahanati hizo ili ziweze kukamilika.

Mwenyekiti aliagiza mkaguzi wa ndani kuhakikisha anafanya ukaguzi wa mara kwa mara katiika miradi ili kuhakikisha kunakua na thamani ya fedha pamoja na kumuelekeza mhandisi kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuweza kuhakikisha tunamuunga mkono mheshimiwa raisi kwa vitendo katika juhudi za kuliendeleza Taifa letu.


Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa