• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

NANAUKA AIPONGEZA MISSENYI KUTAMBUA UMUHIMU WA VIJANA KATIKA UKUAJI WA UCHUMI

Posted on: January 26th, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa namna inavyothamini na kutambua umuhimu wa Vijana katika maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Akiwa katika ziara yake Wilayani Missenyi jana tarehe 25/01/2026 Waziri Nanauka ameipongeza Halmashauri kwa kuandaa programu za mafunzo kwa vijana zinazowasaidia kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii zinazowakabili Vijana.

Sambamba na hilo, aliongezea kuwa amefurahishwa na suala la Halmashauri kuwa na Kanzi Data inayosaidia kutambua idadi ya Vijana wasio na ajira rasmi ndani ya Halmashauri na kuangalia namna bora ya kuwasaidia.

Aidha, alibainisha kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekusudia kuwainua Vijana kiuchumi huku moja ya ajenda yake ikiwa ni kuwatoa Vijana kuwa watu wanaofanya shughuli za uchuuzi na usambazaji na badala yake waingie katika uzalishaji na utekelezaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bi. Seraphina Rwegasira alieleza kuwa katika kutekeleza shughuli za maendeleo ya Vijana, jumla ya maeneo yenye ukubwa wa hekta 1,068 yametengwa kwaajili ya shughuli za kilimo kwa vijana. Huku akibainisha maeneo hayo kuwa ni Kyakakera lililopo Kata Kyaka hekta 163, Buturage lililopo Kata Bugandika hekta 631 na Kafunjo lililopo Kata Buyango hekta 274.

Aliongezea kuwa, makongamano 43 yaliyowahusisha Vijana 9,563 kutoka Kata zote 20 yameendeshwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kuwawezesha Vijana kubainisha changamoto zinazowakabili na namna wanavyoweza kuzitatua kwa kutumia fursa za kiuchumi na kijamii zilizopo ndani na nje ya Wilaya.

Kwa upande wao Vijana Wilayani Missenyi wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa namna wanavyoendelea kuwapambania Vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Joel Nanauka alitembelea Kiwanda cha Vijana cha Chaki (Missenyi Standard Chalks) na Kiwanda cha Vijana cha uzalishaji wa unga wa lishe (Missenyi Nutritional Flour Group) na kuona shughuli za uzalishaji zinazofanywa na vijana.

Ziara hiyo ilienda sambamba na zoezi la ugawaji wa vifaa kwa vijana kutoka makundi maalum ambapo vikundi 15 vilipokea vifaa hivyo ambavyo ni Cherehani 16 za kawaida, Mashine kubwa ya kukaushia nywele saluni (Dryer) 3, Mashine ndogo za kukaushia nywele saluni (Dryer) 7, Cherehani za kudarizi 3, Majiko matatu ya gesi, Mitungi mitatu ya gesi, Mashine moja ya kuchomelea vyuma na Mashine moja ya kutengeneza sweta.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 05, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MUDA (MKATABA) YA UDEREVA November 19, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MWANDISHI MWENDESHA OFISI, MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU NA DEREVA November 14, 2025
  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA WATENDAJI WA UCHAGUZI NGAZI YA VITUO October 22, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NANAUKA AIPONGEZA MISSENYI KUTAMBUA UMUHIMU WA VIJANA KATIKA UKUAJI WA UCHUMI

    January 26, 2026
  • WALIMU MISSENYI WAPATIWA MAFUNZO KUWAHUDUMIA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

    January 16, 2026
  • WADAU WA MAENDELEO MISSENYI WAPEWA ELIMU KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE

    January 13, 2026
  • DC MAIGA AWATAKA WAZAZI WASICHOKE KUWAPA WATOTO MLO KAMILI

    November 20, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa