• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WALIMU MISSENYI WAPATIWA MAFUNZO KUWAHUDUMIA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

Posted on: January 16th, 2026

Wakuu wa Shule na Walimu Walezi wa Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule za Sekondari Wilayani Missenyi, leo tarehe 16/01/2026 wamepatiwa mafunzo ya elimu jumuishi ya namna ya kuwahudumia Wanafunzi wote bila kujali tofauti zao za kimwili, kiakili, kijamii na kiuchumi katika Shule zao.

Akifungua mafunzo hayo katika Ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. John Paul Wanga amesema kwamba, mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha Walimu wajibu wao katika kuhakikisha kila mwanafunzi anapata fursa sawa ya kujifunza, bila kujali changamoto ya ujifunzaji aliyonayo mwanafunzi.

Ameongezea kuwa kupitia mafunzo hayo Walimu watajengewa uwezo kuhusu mbinu za ubainishaji na utambuzi wa Wanafunzi wenye ulemavu, na mbinu za utoaji wa afua stahiki kwa Wanafunzi wenye ulemavu.

Aidha, Bw. John Wanga amewaelekeza Wakuu wote wa Shule kuhakikisha kila Shule inafanya zoezi la ubainishaji na utambuzi wa Wanafunzi wenye mahitaji maalum kabla ya tarehe 31/03/2026.

Pia ameelekeza kila Shule ihakikishe Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapewa afua stahiki kama vile vifaa vya kujifunzia, madawati na miundombinu rafiki.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Mwl. Morega Mongate ameahidi kusimamia na kuhakikisha Walimu waliopatiwa mafunzo wanatekeleza ipasavyo majukumu yao kwa kuzingatia yale yote waliyofundishwa katika mafunzo hayo.

Takwimu zinaonesha Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma elimu ya Sekondari Wilayani Missenyi ni 79, kati ya hao Wanafunzi 58 wanasoma nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na 21 wanasoma katika Shule za Sekondari 31 zilipo ndani ya Halmashauri.

Aidha, wapo baadhi ya Wanafunzi wenye dalili za ulemavu katika Shule ambao hawajatambuliwa, hivyo katika kutatua changamoto hiyo na changamoto ya uhaba wa Wataalamu wa Elimu maalum, Halmashauri imeandaa mafunzo hayo kupitia Wataalamu waliopo ambapo kila Shule imewakilishwa na Walimu wawili.

Mafunzo hayo ya Elimu jumuishi yameenda sambamba na ziara ya mafunzo katika Kitengo cha Elimu maalum kilichopo Shule ya Msingi Bunazi, ambapo pia Walimu hao wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule hiyo.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 05, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MUDA (MKATABA) YA UDEREVA November 19, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MWANDISHI MWENDESHA OFISI, MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU NA DEREVA November 14, 2025
  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA WATENDAJI WA UCHAGUZI NGAZI YA VITUO October 22, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIMU MISSENYI WAPATIWA MAFUNZO KUWAHUDUMIA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

    January 16, 2026
  • WADAU WA MAENDELEO MISSENYI WAPEWA ELIMU KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE

    January 13, 2026
  • DC MAIGA AWATAKA WAZAZI WASICHOKE KUWAPA WATOTO MLO KAMILI

    November 20, 2025
  • DED MISSENYI ALETA KLINIKI YA ARDHI KATIKA KATA YA KYAKA NA MUTUKULA

    November 19, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa