• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WATAALAMU WA MIFUGO, WAFUGAJI WAJENGEWA UWEZO

Posted on: May 18th, 2018

Wataalamu wa mifugo wilayani hapa wamejengewa uwezo wa namna bora ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa. Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na mradi wa North South Trans-border Project (NSTP)yamefanywa na wataalamu Ndg Gidi Smolder na Ndg. Yvonne Robber Kutoka Nchi ya Uholanzi. 

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku nne mfululizo yakihusisha  wataalamu wa mifugo waliopo makao makuu ya wilaya, wataalamu wa mifugo wa kata na vijiji, wawakilishi wa mitandao ya wafugaji wa tarafa za Missenyi na Kiziba pamoja na baadhi ya wafugaji waliopata fursa hiyo.  Aidha, mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili mfululizo katika eneo la Bunazi kwa kata za Kassambya, Minziro, Mutukula, Kyaka na Kilimilile na siku mbili mfulululizo katika kituo cha rasilimali za wakulima Kitobo kwa Kata za Kitobo, Bwanjai, Buyango, Ishozi, Ishunju na Gera.

Wakiwa katika vituo mbalimbali vya mafunzo , wafugaji wamepewa mafunzo mbalimbali yaliyohusu  njia bora za ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa lengo la kufanya kifanya ufugaji wa kibiashara. “Tumefarahia sana ujio wa wataalamu hawa, tumepata elimu ambayo hatukuwa nayo hapo kabla… ndio pamoja na changamoto ya lugha lakini nimepata kitu.”  Alisikika akisema mmoja wa wakilishi wa mtandao wa wafugaji wanawake Missenyi. Pia wafugaji hao hawakusita kuzitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wafugaji katika eneo la Missenyi ni  uhaba wa malisho ya mifugo.

Wakizungumza na tovuti hii, mara baada ya mafunzo hayo wakufunzi wamewataka wafugaji waliopo katika wilaya hii kuitumia vizuri fursa ya hali ya hewa rafiki kwa mifugo iliyopo katika eneo la missenyi kwa kufanya ufugaji bora na wakisasa wa ng’ombe wa maziwa na pia kutambua wataalamu waliopo na kuwatumia ipasavyo. “Maeneo haya yana kijani cha kutosha, maeneo yote Kagera na hapa Missenyi hali ya hewa yake ni rafiki kwa mifugo sio kama sehemu zingine, wafugaji wa maeneo haya wanachohitaji ni elimu tu na si kungine…hata wewe nakushauri kama huna mifugo fikiria kufuga” alisema Ndg. Gidi Smolder . 

Nae mtaalamu wa Mifugo kutoka kutoka makao makuu ya Wilaya ndugu Jasson Rwazo hakusita kutaja changamoto inayo wakabili wafugaji ni pamoja na Wafugaji kutumia majani ya asili yasiyo na virutubisho vya kutosha hivyo kusababisha ng’ombe kutoingia katika joto kwa wakati na uzalishaji wa maziwa kupungua huku gharama za utunzaji zikibaki kuwa kubwa. Sambamba na hilo amewataka wafugaji wa eneo hili wafuge kibiashara kwa kutumia mbinu bora za ufugaji wa kisasa na wasifuge kimazoea. “Pamoja na changamoto walizonazo, wafugaji wetu wanatakiwa wabadilike, waache kufuga ili mradi wanafuga wanatakiwa wawekeze katika ufugaji ili waone faida zake” alimalizia Bwana Rwazo.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa