• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

Posted on: April 26th, 2025

Wananchi Wilayani Missenyi, Mkoani Kagera waaswa kuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa vitendo kwa kukemea dalili zozote zenye nia ya kuuvunja muungano.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga leo Aprili 26, 2025 wakati wa maadhimisho ya sherehe ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Wananchi sote kwa pamoja na kila mpenda maendeleo, kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa kuenzi Muungano huu kwa vitendo kwa kukemea dalili zozote zenye nia ya kuuvunja muungano huu". Amesema Mhe. Maiga.

Ameongezea kuwa njia moja wapo ya kuwaenzi Waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuudumisha muungano ambao ni urithi wa aina yake waliotuachia Waasisi wa muungano huu.

Aidha, amewataka Wanamissenyi na Watanzania wote nchini kuuenzi Muungano kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha utendaji wa mazoea.

"Watanzania inatupasa tuuenzi Muungano wetu kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, kujitolea na kuacha utendaji wa mazoea, tuadhimishe miaka 61 ya Muungano kwa kuudumisha na kufanya kazi kwa bidii". Amesema Mhe. Maiga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mhe. Projestus Tegamaisho amewataka Wanamissenyi kutumia Muungano huu kama fursa ya kukua kiuchumi hasa kwa wafanyabiashara.

"Wanamissenyi tembeeni mpaka Zanzibar kule kuna bidhaa za ajabu, kwahiyo tunaweza tukawa na bidhaa kutoka Zanzibar katika Gulio letu la Bunazi zikaenda mpaka Uganda na maeneo mengine bila kutegemea Uganda kuleta huku kila siku". Amesema Mhe. Tegamaisho.

Maadhimisho haya ya sherehe ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wilayani Missenyi yamefanyika katika viwanja vya Gulio la Bunazi yakiambatana na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na upandaji miti katika Shule ya Msingi Bunazi 'B', matembezi ya amani ya Muungano, usafi wa mazingira katika Gulio la Bunazi, mashindano ya uandishi wa Insha kwa wanafunzi, pamoja na mashindano ya mpira wa miguu.

Aidha, kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka 2025 inasema; Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. "Muungano wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025".

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa