• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI WABORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA SHULENI

Posted on: March 10th, 2023

Ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za maendeleo katika Kata ya Kassambya iliopo Wilaya Missenyi Mkoani Kagera  umekua nyenzo muhimu katika  maendeleo haswa katika sekta ya elimu kutokana na jamii kuwa muitikio chanya katika kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za maendeleo katika Kata ya Kassambya ulianzia ngazi ya jamii katika mikutano ya vijiji na vitongoji haswa katika upangaji mikakati na kuibua vipaumbele kuilingana na matakwa ya jamii ili jamii kuweza kujiona kwamba wao ni wamiliki na wao ni sehemu ya mradi wanaokwenda kufanya utekelezaji katika maeneo yao.

Katika shule ya sekondari Bunazi iliopo katika Kata ya Kassambya katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi mnamo mwaka 2018 kupitia mikutano ya vijiji wananchi waliamua kuibua mradi wa ujenzi wa  vyumba 02 vya madarasa ili kukabiliana na  ongezeko kubwa la wanafunzi katika shule ya sekondari Bunazi kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

Pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa jamii iliadhimia kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunzia ili kuongeza ufaulu katika shule ya sekondari Bunazi ikiwa ni Pamoja na kuboresha mazingira ya walimu na wanafunzi  ili yawe rafiki kwa lengo la kuinua taaluma shuleni hapo.

Ili kuonyesha uhitaji  huduma Fulani katika jamii kupitia mchakato wa kuboresha fursa na vikwazo kwa maendeleo, wananchi wanapaswa hushirikiana katika hatua za awali zikiwemo  kuhakikisha wanatafuta eneo la ujenzi na kuanza ujenzi mpaka kufikisha jengo hatua ya boma kisha serikali inauchukua mradi husika na kufanya umaliziaji wake mpaka hatua ya mwisho baada ya wananchi wenyewe kuonyesha uhitaji wake.

Katika mikutanio ya hadhara inayoendeshwana Mkuu wa wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali Wilson Sakulo kwa Kata zote 20 za Wilaya ya Missenyi wakati akiwa katika Kata ya Kitobo terehe 09 Machi 2023 aliwasihi wananchi wa Missenyi juu ya njia moja wapo ya kumaliza changamoto ya miundo mbinu shuleni ni pamoja na kuhakikisha waanchi wao wenyeewe wanajituma na kujenga jengo hadi kufikia hatua ya boma kisha seriakli kufanya umaliziaji wa jengo husika kwa asilimia 100.

Kwa upande wa Makamu Mkuuu wa shule ya sekondari Bunazi Mwl. Iddy Yusuph Hanyaga ni kwamba baada ya shule hii kutoka kwenye umiliki binafsi na kuwa shule ya serikali miundo mbinu yake ilikua chakavu hali iliosabababisha kuona kwamba kuna uhitaji wa kuboresha mazingira ili yawe rafiki katika kujifunza ambapo iliwabidi kuanza kushirikisha jamii katika kutatua changamoto ya miundo mbinu katika shule.

Kutokana na ongezeko la mbiundo mbinu mashuleni kupitia nguvu za jamiii na serikali vipo vyumba vilivyojengwa kipindi cha nyuma lakini kwa kipindi cha hivi karibuni mazingira yamekua bora zaidi haswa ukiangalia vyumba vipya viwili vilivyojengwa kupitia nguvu za jamii  mpaka hatua ya boma na serikali  kumazia mwaka 2022 kwa 100%,  vyumba vingine viwili  vilivyojengwa na serikali kupitia miradi ya UVIKO19 mwaka 2021 na ongezeko la chumba kimoja cha darasa  kilichojengwa kwa ajili ya kidato cha kwanza 2023 na kufanya shule kuwa na jumla ya vyumba vitano vipya kwa kipindi kifupi.

‘’Kutokana na ongezeko la miundo mbinu ya kujifunzia haswa vyumba vya madarasa na madawati shule ya sekondari Bunazi imeweza kupokea wanafunzi wengi zaidi ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo tulikua tunapokea wanafunzi 100 lakina mfwaka 2022 tulipokea kidato cha kwanza wanafunzi 462, mwaka 2023 wanafunzi 562 na kwasasa ukiongeza wanafunzi wanao hamia kidato cha kwanza tuu wanafikia 600. Alisema Mwl. Iddy.

Makamu mkuu wa shule alisisitiza kwamba hali ya ufaulu shuleni imekua ikongezeka kadri miundo mbinu inavyo enbdelea kuongezeka na kuboreshwa mfano mwaka 2017 na 2018 ufaulu ulifikia 84% ukulinganisha na mwaka 2019 na 2020 ambapo ufaulu ulifikia 92% kwa kidato cha pili na kwa upande wa kidato cha nne mwaka 2020 ufaulu ulikua 75%, mwaka 2021 ufaulu ulikua 84% na mwaka 2022 ufaulu ulikua 90%.

‘’kutokana na mazingira mazuri ya shule kwa sasa tuna wanafunzi wanao anzia hapa kidato cha kwanza na pindi wanapomaliza kidato cha nne wanarudi hapa kuendelea kidato cha tano hivyo ni furaha kwetu sisi walimu kuona mtoto anaanza hapa kidato cha kwanza na kumalizia hapa kidato cha sita’’ alisema Mwl. Iddy

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Kata ya Kassambya Abdulrauf Khalid Athumani alisema kutokana na ushirikishwaji mzuri wa wananchi wa Kata Kassambya kwasasa waandelea kushirikiana katika ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya Sekondari Bunazi ili kuwezeha walimu kuishi mazingira ya karibu na maeneo ya shule hali itakayo ongeza ufaulu kwa wanafunzi kwani tutakua tumewaboreshea walimu mazingiora ya kufanyia kazi Pamoja na kupata muda mzuri Zaidi wa kuwaangalia wanafunzi.

Kwa upande wake Sophia Kombo  ambaye ni  mmoja wa wanafunzi ambao walianzia kidato cha kwanza shuleni hapo na sasa yupo kidato cha Tano alisema nikweli kwamba miundo mbinu haswa majengo na madawati vimeongezeka sana miaka ya hivi karibuni Pamoja na  kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwani madarasa mengi yamekua mapya na madawati mengine wamewapunguzia madara mengine ukilinganisha na hapo awali ambapo vyumba vilikua havitoshelezi lakini kwa sasa wanakaa kwa nafasi na majengo ya sasa yana madirisha makubwa yanayoingiza mwanga wa kutosha tofauti na yale ya zamani.

Dhana ya ushirikishwaji mzuri wa jamii katika kata ya Kassambya umeongeza hali ya umiliki wa  miradi kuwa ni ya jamii kwa ujumla na sio serikali pekee hali inayosaidia  miradi kuwa salama na endelevu kwa kua kila mwananchi kuhakikisha anautunza kama wake kutokana na ile hali ya ushirikishwaji katika hatua za kupanga na si katika utekelezaji tuu.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa