• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA MISSENYI

Posted on: May 16th, 2025

Leo Mei 16, 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imeadhimisha siku ya Wauguzi Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 ya Mwezi Mei Duniani kote.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo zilizofanyika katika Ukumbi wa Nyabutaizi uliopo Wilayani Missenyi, Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Bi. Lucia Eustace amesema kwamba Siku ya Wauguzi Duniani ni siku muhimu Duniani kote ambapo wanatambua, kuthamini na kusherehekea mchango mkubwa wa Wauguzi katika Wilaya ya Missenyi, Taifa la Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla.

Ameongezea kuwa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Uuguzi Nguvu ya Mabadiliko" inaakisi mchango mkubwa unaotolewa na Wauguzi na kuwataka waendelee kuzingatia maadili ya taaluma yao.

"Katika sekta ya Afya inayofanya shughuli za kinga na tiba asilimia 80 ni nguvu ya Wauguzi, kwahiyo kauli mbiu tunayotembea nayo mwaka huu tuna imani Wauguzi wakibaki ndani ya maadili ya taaluma yao na maadili ya utumishi, tuna imani pia taaluma zote za kada ya Afya wataenda kubadilika kwa kutoa huduma bora kwa mteja", amesema Bi. Lucia.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amesema kwamba maadhimisho ya Siku ya Wauguzi huadhimishwa tarehe 12 Mei kila mwaka Duniani kote, lakini kutokana na mwingiliano wa kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi inafanya maadhimisho haya muhimu kwa Wauguzi leo Mei 16, 2025.

Pia, amewataka Wauguzi kuifanya siku hii kuwa ndio mwaka mpya wa kiuguzi kwa kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyao.

"Katika siku hii ya leo uwe ndio mwaka mpya wa kiuguzi wa kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyenu kwa upendo, kujituma, kujitolea, ubunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kutoa huduma inayokusudiwa kwa kuepuka mambo yote yanayoharibu taswira ya utoaji huduma bora na zenye staha", amesema Mhe. Maiga.

Aidha, kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. Egidius Kahendaguza amewataka Wauguzi kuwa wema na si wabaya kwa wanaowahudumia.

"Msikubali kuwa katika upande wa Wauguzi wabaya, tukiwa kwenye njia ya Wauguzi wema watu wote watapata faraja na Mwenyezi Mungu atajidhihirisha uponyaji utafanyika na maisha yataendelea", amesema Bw. Kahendaguza.

Akitoa neno la shukrani Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Missenyi Dkt. Jamily Yahaya amesema kuwa Halmashauri inatambua umuhimu wa Wauguzi na inawatambua kama Wauguzi kama moyo wa Idara ya Afya.

Ameongezea kuwa Halmashauri itaendelea kusimamia stahiki za Wauguzi na maadili ya Wauguzi katika kazi.

"Sisi kama Halmashauri tutaendelea kusimamia stahiki zenu Wauguzi lakini pia tutaendelea kuwasimamia na kuwaelekeza katika kukumbushana umuhimu wa maadili ya taaluma zetu lakini pia mafunzo mbalimbali ili kujengeana ujuzi", amesema Dkt. Jamily.

Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka Mei 12, Duniani kote ikiwa ni kumbukumbu kwa muasisi wa huduma ya Uuguzi Florence Nightngale ambaye alikuwa Muitaliano aliyezaliwa mwaka 1871.

Kwa mwaka huu 2025 maadhimisho ya siku ya Wauguzi Wilayani Missenyi yameambatana na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa vyeti na zawadi kwa Wauguzi wastaafu na Wafanyakazi bora katika kada ya Uuguzi, kuwatembelea wagonjwa katika Kituo cha Afya Bunazi, pia matembezi ya amani na burudani mbalimbali.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA MISSENYI

    May 16, 2025
  • WATENDAJI KATA NA VIJIJI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTOA ELIMU YA LISHE KWA JAMII

    May 14, 2025
  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa