• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

LAAC YAPONGEZA UBORA MIUNDOMBINU YA HOSPITALI YA WILAYA YA MISSENYI

Posted on: March 17th, 2024

Kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) leo tarehe 17 Machi, 2024 imefanya ziara ya siku moja kwa ajili ya ukaguzi wa miradi miwili inayoendelea kujengwa ambayo Mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Missenyi na ujenzi wa shule ya sekondari Kitobo.

Katika ukaguzi huo kamati imepongeza hatua nzuri zilizofikiwa pamoja na kupongeza usimamizi mzuri wa ujenzi wa miundombinu uliokidhi ubora na viwango katika ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Missenyi na thamani ya fedha inaonekana.

Aidha kamati hio inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali za Mitaa Mhe. Stanslaus Mabula imeagiza kuhakikisha maeneo yote yaliyojengwa miradi hio miwili yanafanyiwa tathmini ya kimazingira ili kuwa na uhakika juu ya kudumu kwa miundombinu inayojengwa na serikali katika maeneo hayo.

Akiongoza kikao cha Kamati hio kwaniaba ya makamu mwenyekiti, Mhe. Daimu Mpakate ambaye ni Mbunge wa Tunduru Kusini ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kuandikia barua Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuwaomba wakati wa utekelezaji wa miradi waweze kupatiwa kiasi cha fedha tofauti na Halmashauri zingine kwani kulingana na mazingira ya Missenyi inabidi utumie gharama nyingi tofauti na maeneo mengine katika Msingi wa nyumba pamoja na kuongeza ubora ili kukabiliana na athari zitokanazo na tetemeko la ardhi.

‘’Hakikisheni mnatumia mapato ya ndani pia kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali kama shule ya Sekondari Kitobo na Hospitali ya Wilaya ya Missenyi ili majengo yatumike ipasavyo kutoa huduma kwa jamii kama ilivyokusudiwa’’ Alisema Mhe. Mpakate.

Mpakate pia ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwaniaba ya Kamati hiyo kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo kikamilifu ili kiwango cha fedha kinachotumika kiendane na ubora wa majengo yanayojengwa kama ilivyofanyika vizuri katika Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Missenyi.

Aidha, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa imetoa siku moja kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera kuainisha madai yote ya vifaa na vifaa tiba wanavyovidai katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwani katika maeneo mengi waliyoyatembele wamekuta madai ya vifaa na vifaa tiba vya thamani kubwa na vyenye muda mrefu bila kufikishwa maeneo husika.

“Niangize halmashauri zote za Mkoa wa Kagera kuainisha madai yote wanayodai MSD hadi ifikapo kesho wakati wa kufanya majumuisho ili kamati ijiridhishe na kuelekeza yashughulikiwe kwa wakati.” Alisema Mhe. Mabula.

Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Kagera Kalendero Masatu amesema, MSD imefanya maboresho makubwa ya kusambaza bidhaa za afya ambazo halmashauri za mkoa wa Kagera zinaidai MSD kuanzia mwaka 2021/23.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt.Charles Mahera amesema TAMISEMI itaendelea kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa nchi nzima ili ziweze kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili thamani ya fedha iendane na miradi inayotekelezwa.


Kamati hii imefanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Missenyi ambapo Wilaya ya Missenyi imeipokea kamati hii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na siku ya terehe 18 Machi, 2024 kamati hio inaendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.


Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa