• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

KUIMARISHA MIFUMO YA SEKTA YA UMMA , UTAWA BORA NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI WILAYA YA MISSENYI

Posted on: November 17th, 2022

Kupitia mradi PS3+ unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) umeendelea kuimarisha shughuli ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma kwa ajili ya kuweka mifumo ya sekta ya umma inayokidhi mahitaji ya wananchi ili kuleta  ubora wa huduma muhimu za umma katika ngazi ya mitaa.

Hayo yamebainika baada wataaalamu wa mradi huo kufanya ufuatiliaji juu ya mafanikio na mabadiliko yatokanayo na utolewaji wa mafunzo hayo leo tarehe 16/11/2022 ili kufanya tathmini katika maeneo mbali mbali ya kutolea huduma katika Kata ya Kassambya na Kanyigo.

Katika kata ya Kassambya walitembelea shule ya sekondari Bunazi, shule ya msingi Kassambya, Kituo cha Afya cha Bunazi, ofisi ya kijiji Bunazi na Omundongo na Kata Kanyigo walitembelea Shule ya msingi  Nshumba, Zahanati ya Kikukwe na ofisi ya kata Kanyigo.

Kwa upande wake Suma Kaare ambaye ni mkuu wa kitego cha Utawala bora na Ushirikishwaji wa wananchi katika mradi wa PS3+ makao makuu Dar es salaam alisema Natamani kujua kama matamanio ya serikali yanatimia ikiwemo uwepo wa mifumo na ufanyaji kazi, utolewaji wa taaarifa na kubandikwa kama ilivyotolewa kwenye mfumo na itakua vyema kama kamati za vituo hivi kama zipo na zinafanya kazi ikiwemo kujadili taarifa za mapato na mtumizi ya kituo bila kusahau uwepo sanduku la maoni na linafunguliwa mara ngapi na namna gani wanashughulikia malamiko au maoni ya wananchi kwa ajili ya kuleta utawala bora na ushirikishwaji.

Mafunzo haya  yalijumuisha Watendaji wa kata, Waganga wafawidhi wa vituo vya afya na zahanati na watendaji waliopata mafunzo walielekezwa kutoa mafunzo kwa wataalamu waliopo ofisi za kata na watendaji wa vijiji ikiwemo kutumia mfumo wa kielektoniki wa MUKI kupitia chuo cha serikali  za mitaa LGTI Dodoma.

Kwa upande vituo vya afya, zahanati, shule za msingi na sekondari waliweza kufanya ufuatiliaji juu ya utumikaji wa wa mifumo kama GoTHOMIS kwa sehemu za kutolea huduma za afya na FFARS kwa shule za msingi na sekondari, utolewaji wa taarifa mbalimbali za mifumo na taarifa zinginezo na kuwekwa wazi kupitia mbao za matangazo, mikutano ya vijiji ili kuhakikisha jamii nzima inayozunguka taasisi husika inapata taaifa za msingi ikiwemo kushirikishwa katika mambo mbalimbali ikiwemo uwekaji wazi wa taarifa za mapato na matumizi ya taasisi husika katika mbao za matangazo, uwepo wa masanduku ya maoni utumikaji wake na ufanyikaji wa vikao vya kisheria katika vituo na maeneo ya serikali za mitaa haswa katika vijiji na kata.

Aidha kwa upande wa mratibu wa mradi wa PS3+ kanda ya ziwa Bw. Pelestian Masai aliwakumbusha kwamba mnamo mwezi mei 2022 walikutana na watendaji wa kata na hivyo kwa upande wa serikali za mitaa ufuatiliaji unafanyika katika utiririshaji wa mafunzo kutoka kwa watendaji wa kata kwenda kwa wagani wa kata, watendaji wa vijiji juu ya utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi na kuweza kufikia hatua ya kupata vyeti kwa wale walio hitimu mafunzo.

Kwa upande wake Dk. Mary Kasonka ambaye katika mradi ni mshauri wa maswala ya uatawa bora na ushirikishwaji wa jamii alisisitiza katika Utolewaji wa taarifa za msingi haswa za mapato na matumizi, uwekwaji wa masanduku ya maoni, matumizi ya mbao za matangazo katika ofisi za umma ili kuongeza ushirikiano wa wananchi katika shughuli mbalimbali.

Mradi wa PS3+ Umelenga kuimarisha mifumo ya sekta ya umma haswa katika uboreshaji, upangaji na usimamizi unaozingatia ushahidi wa huduma za umma katika ngazi ya mtaa, Kuimarisha utawala wa ndani kupitia ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli mbalimbali na uwajibikaji wa kijamii na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na matumizi ya uwazi ya rasilimali fedha katika shughuli mbalimbali.


Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa