• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AZINDUA RASMI UJENZI WA MRADI WA MAJI WA KYAKA-BUNAZI

Posted on: June 1st, 2020

Katibu Mkuu  wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amezindua rasmi ujenzi wa mradi wa maji wa Kyaka-Bunazi unaotegemewa kuanza hivi karibuni. Akiongea na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika Ukumbi wa William Katunzi uliopo wilayani hapa, katibu mkuu amesema amepata furaha ya pekee kuzindua mradi huu mkubwa ukiwa ni mradi wa kwanza Tanzania unaotumia maji ya Mto kagera.

Mradi huu wa unatarajiwa kutumia kiasi cha Tsh. Bilioni 15.1 zote zikiwa ni fedha za ndani ambapo kiasi cha Tsh. Milioni 650 zimeshatengwa tayari. Mradi huu ni moja ya miradi ipatayo 10 inayotekelezwa katika miji 13 ya kanda ya ziwa.

Katibu mkuu hakusita kuelezea umuhimu wa mradi huu kwa kutaja sababu kuu tatu zilizopelekea kutekeleza mradi huu ambazo ni Miji ya Kyaka na Bunazi kutokuwa na maji kabisa, pili kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Joseph Pombe Magufuri na tatu hali ya mradi huu kuwa wa kwanza wa Serikali kutumia maji yamto Kagera.

Katika utekelezaji wa mradi huu, katibu mkuu amesema hatua za ujenzi wa mradi umegawanyika katika hatua kuu mbili ambapo hatua ya kwanza itahusisha shughuri kama ujenzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa tenki kubwa la maji, kutengeneza mtambo wa kuchuja na kusafisha maji pamoja na kutandaza bomba kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye tanki. Hatua hii inataraji kugharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 9.4. Hatua ya pili itahusisha ujenzi wa mtandao wa usambazaji wa maji kwa wananchi kutoka kwenye tanki kuu ambapo hatua hii itagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 5.7

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kyaka Mh. Projestus Tegamaisho amekiri kupokea mradi huu kwa namna ya pekee huku akiwataka wananchi wa Kyaka na vitongoji vyake kuupokea na kuulinda kwa nguvu zao zote  kwani si tu utamtua mwanamke ndoo kichwani bali ni fursa kwao pia kwa kuwa utawainua kiuchumi kutokana na matumizi ya maji katika kilimo na shughuli mbalimbali za kijamii huku akiimwagia sifa serikali ya awamu ya Tano kuwa ndio serikali ambayo imevunja rekodi kwa kufanikisha kupeleka maji kwa wananchi kutoka mto Kagera.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ndugu Innocent Mukandala ameishukuru Serikali kwa kuruhusu utekelezaji wa mradi huu kwani utakuwa suluhisho kubwa la tatizo la maji katika maeneo yote yatakayofikiwa na mradi kwani kwa sasa hali ya mtandao wa maji kwa Wilaya ya Missenyi ni asilimia 62 huku akiwashukuru pia wadau wa maendeleo kama World vision kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji vijijini.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa kijiji cha Bulifani ambacho ndipo patakaopjengwa chanzo kikuu cha maji ameishukuru serikali kwa kuleta mradi huu mkubwa katika maeneo hayo huku akimuomba mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi kutumia vijana wa maeneo yanayozunguka mradi na si kuleta watu kutoka nje hata kwa kazi wanazoweza kufanya.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa