• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

JAMII IONGEZE JITIHADA KATIKA KUTOKOMEZA UKIMWI

Posted on: December 1st, 2023

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewaongoza wanachi wa Mkoa wa Kagera katika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani leo tarehe 01/12/2023 ambapo maadhimisho haya yamefanyika Kimkoa katika Viwanja vya kiwanda cha Kagera Sukari kilichopo Kata ya Nsunga wilaya ya Missenyi.


Akizungumza na wanachi wanachi wa Mkoa wa Kagera Mhe. Mwassa alisema lengo la maadhimisho haya kuwanguanisha wanajamii kote ulimwenguni ili kuendeleza mapambano dhidi ya kutokomeza tatizo la UKIMWI lililopo Duniani kote.


"Siku hii hutoa fursa kwa jamii yote, watu waliothirika  na virusi vya UKIMWI wakiwemo wagane,wajane, watoto  yatima ili kufarijiwa, kukutana na kutafakari athari za janga la UKIMWI na changamoto mbalimbali za kiafya zinazoendele kuwakabili Wananchi walioathirika na wale ambao hawajaathirkia katika kuboresha afya ya jamii ili kuleta maendeleo" .Alisema Hajjat Mwassa.


Aidha aliwasihi wananchi kwamba bado suala la UKIMWI limeendelea kuwa zito pamoja na kuendelea kuleta athari za kujidhihirisha kijamii, kiuchumi na kiafya hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari kwani changamoto zitokanazo na mahusiano ya kingono ni nyingi na sio UKIMWI peke yake.


Kwaupande wake Bw. Issa Mrimi ambaye ni mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Kagera akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya UKIMWI Mkoa wa Kagera kwaniaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera alisema hali ya maambukizi Mapya kwasasa Halmashauri ya Wilaya Missenyi ni 2.7%, Bukoba Manispaa 2.3%, Bukoba Vijijini 2.7%, Karagwe 01%, Kyerwa 02%, Muleba 02%, Biharamulo 01% na Ngara 01%.


"Idara ya afya kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kupambana na janga hili ikiwa nki pamoja na kuweka mikakati ya kuibua wale ambao hawajaweza kupima na kujua hali zao haswa kupitia njia ya kupima mshirika mwenza hali ianayosaidia kuwafikia watu wengi zaidi" Alisema Bw. Malimi


Aidha hali ya Maambukizi kwa Mkoa wa Kagera imepungua ukilinganisha na mwaka jana kutokana na afua mbalimbali zinazotekelezwa zilizopelekea kupungua kwa maambukizi ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya jipime, huduma ya dawa kinga na matumizi ya Kondom.


Maadhimisho haya yamehudhuriwa na wanachi wa Wilaya ya Misenyi pamoja na wadau kama MDH, Kagera Sugar, World Vision, Compassion, HUMULIZA, SHINA Tanzania/ITIKA, TADEPA, MHOLA na H-PON.


Maadhimisho haya huadhimishwa kote duniani na nchi wanachama wa umoja wa mataifa kila ifikapo tarehe 01 Disemba ya kila mwaka, Kauli mbiu ya Maadhimisho haya kwa mwaka 2023 ni "JAMII IONGOZE  KUTOKOMEZA  UKIMWI" ambapo kauli mbiu hii inaipa kipaumbele jamii katika kushika hatamu katika kuelekea kutokomeza maambukizi ya UKIMWI ifikapo 2030.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa