• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Secondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Mipango Takwimu na Uuatiliaji
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

Afya na Ustawi wa Jamii

UTANGULIZI

Idara ya Afya ni miongoni mwa Idara katika Halmashauri ya Wilaya Missenyi. Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Huduma hizi zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na kwa njia ya mkoba katika maeneo mbalimbali ya Wilaya .  

  • MAJUKUMU YA IDARA

Idara ya Afya inatekeleza majukumu makuu mawili ambayo ni Afya kinga na Afya tiba. Kupitia Afya tiba idara imelenga kutoa matibabu sahihi kwa gharama nafuu kwa wananchi wa Wilaya ya Missenyi na  za jirani. Afya kinga imelenga kuwakinga wananchi wasipate magonjwa yale ya kuambukiza, yasiyoyakuambukiza pamoja na kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

  • AFYA TIBA

Idara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa V wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi, idara imekuwa ikitekeleza majukumu yafuatayo:

  • Kusimamia manunuzi ya dawa, vitendanishi vya maaabara ,vifaa na vifaa tiba kisha kuvisambaza kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
  • Kutoa huduma za matibabu na uuguzi kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya zikiwemo huduma za upasuaji mkubwa na mdogo. Huduma hizi ni kwa wagonjwa wa nje na wagonjwa wa kulazwa.
  • Kufanya ukaguzi wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
  • Kusajili na kuhuisha maduka ya dawa na vipodozi, kuyafanyia ukaguzi mara kwa mara na kuhakikisha yanafuata sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uanzishaji na uwepo wa maduka hayo
  • Kusimamia pamoja na kuzikagua maabara zote na kuhakikisha zimesajiliwa na zinatoa huduma bora kulingana na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya.
  • Kutoa, kusimamia na kuratibu huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Manispaa . Huduma hizi ni pamoja na uzazi salama, huduma za uzazi wa mpango, huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti. Huduma nyinginezo ni pamoja na huduma za kuzuia ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
  • Kuratibu huduma za kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI. Huduma zitolewazo ni pamoja na matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, huduma za kuchunguza na kutibu magonjwa ya ngono pamoja na huduma za wagonjwa majumbani. Huduma hizi hutolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

AFYA KINGA

  • Idara imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali yanayolenga kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuambukiza. Mojukumu hayo ni pamoja na:
  • Ukaguzi wa nyumba za kuishi na majengo ya biashara kama vile nyumba za kulala wageni,majengo ya kutengeneza na kuuza vyakula ili kuondoa machukizo yanayoweza kuhatarisha afya ya binadamu.
  • Utoaji wa elimu ya afya kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
  • Utoaji wa chanjo kwa magonjwa ya kuambukiza kwa wajawazito na watoto
  • Usimamizi wa afya na usalama mahala pa kazi
  • Usimamizi wa usafi wa Mazingira.

Tarifa Kwa Umma

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MISSENYI December 19, 2020
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE JANUARY 2020 January 09, 2020
  • TAARIFA YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO 2015 – 2020 June 28, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YATOA MKOPO WA TSH. 92,150,000.00 KWA VIKUNDI 15 VYA VIJANA NA WANAWAKE

    October 23, 2020
  • TIMU YA MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YAKAGUA MIRADI 17 YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NDANI YA HALMASHAURI

    October 15, 2020
  • HALMASHAURI YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVu

    September 05, 2020
  • KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AZINDUA RASMI UJENZI WA MRADI WA MAJI WA KYAKA-BUNAZI

    June 01, 2020
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    BUNAZI MISSENYI KAGERA TANZANIA

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 38 KYAKA MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: 0732983531

    Namba ya simu :

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa