• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WATENDAJI KATA NA VIJIJI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTOA ELIMU YA LISHE KWA JAMII

Posted on: May 14th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji Wilayani Missenyi kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya lishe kwa jamii ili kuondokana na tatizo la udumavu.

Hayo ameyasema leo Mei 14, 2025 katika Kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya Kata na Vijiji kwa robo ya tatu ya Januari mpaka Machi 2025.

"Kama tutaendelea kuzalisha vijana ambao ni wadumavu kwa kifupi hatujaitendea haki Missenyi na Tanzania, Hivyo ni waombe kila mtu kwa nafasi yake aweze kutoa elimu kwa jamii juu ya namna bora ya kupambana na udumavu na kuzingatia lishe bora", amesema Mhe. Maiga.

Aidha, ametaka uwepo wa mawasiliano na ushirikiano wa karibu baina ya Afisa lishe waWilaya, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji ili taarifa nyingi zinazohusu masuala ya lishe kwa jamii ziweze kushughulikiwa ikiwa ni pamoja na namna ya kufikisha elimu kwa jamii juu ya lishe na kukumbushana utekelezaji wa majukumu yao.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe ngazi ya Kata na Vijiji kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025, Afisa lishe Wilaya ya Missenyi Bi. Faustina Godwin amesema kwamba katika robo ya tatu watoto 4 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali Wilayani Missenyi na kupatiwa matibabu.

"Watoto hao waliogundulika na utapiamlo mkali walipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Bunazi, Hospitali ya Mugana na Kagera Sugar na wote walipona", amesema Bi. Faustina.

Ameongezea kuwa usimamizi shirikishi umefanyika katika Vituo vya kutolea huduma za Afya vya Ruzinga, Buyango, Kitobo, Bugorora, Buchurago, Bulembo, Nyankere, Mwemage, Kilimilile, Igayaza, Ngando, Bunazi HC, Kabyaile na St. Theresia.

Amebainisha kwamba katika vituo vya kutolea huduma za kliniki, utoaji wa dawa za Madini chuma unaendelea kwa wajawazito na jumla ya Wanawake 11,411 waliohudhuria Kliniki wamepatiwa dawa kinga dhidi ya upungufu wa damu na vilema kwa Watoto.

Pia elimu juu ya ulishaji wa Watoto wadogo na wachanga inaendelea kutolewa katika huduma ya mama na mtoto na Mkoba ambapo Wanawake 25,446 walifikiwa kwa kipindi hicho.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Lishe Mkoa wa Kagera Bi. Winifrida Lyoba amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuitumia  elimu hii wanayopata kuisaidia jamii juu ya masuala ya lishe.

"Watendaji wa Kata na Vijiji tumieni nafasi hii kufikisha taarifa hizi kwenye jamii, ili kuweza kuikomboa dhidi ya udumavu", amesema Bi. Winifrida.

Ameongezea kuwa watu wengi wanasumbuliwa na udumavu na ni vyema kukubali hilo ili kuweza kupambania Watoto wetu na kuchukua hatua.

Kikao hicho cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya Kata na Vijiji kwa robo ya tatu kimefanyika katika Ukumbi wa William F. Katunzi uliopo Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kuhudhuriwa na Wajumbe kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Wakuu wa Idara zinazohusika na lishe, Afisa Lishe Mkoa, Watendaji wa Kata na Vijiji, Maafisa Tarafa, Wajumbe Timu ya Menejimenti ya  Afya ya Wilaya (CHMT) na Watoa huduma za Afya.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • WAZAZI WAHIMIZWA KUSHIRIKI KAMPENI YA UTOAJI WA MATONE YA VITAMINI A

    June 05, 2025
  • UFUNGUZI SOKO LA NDIZI NA STENDI GERA, NEEMA KWA WANANCHI WILAYANI MISSENYI

    May 31, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa