• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

Posted on: April 30th, 2025

Leo terehe 30 Aprili, 2025 Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi limeelekeza kufanyika zoezi la utaoji elimu kwa wale wote waliokosa Mkopo unaotolewa na Halmashauri kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Hayo yamesemwa katika mkutano  wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa robo ya tatu 2024/25 uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Wiliam F. Katunzi uliopo makao makuu ya Halmashauri.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mhe. Projestus Tegamaisho amesema kwamba waliokosa hawajafahamu sababu za kukosa mkopo uliotolewa awamu ya kwanza hivyo kabla ya kuanza zoezi kwa awamu ya pili elimu itangulie ili waweze kujua walikosea wapi na kufanya masahihisho ili kufanikiwa katika awamu ijayo.

"Vikundi vingi wana maandiko ya mradi lakini hawajui kilichopo kwenye andiko na pale wakaguzi wanapowatembelea wakiulizwa maswali wanashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na wengi wao kuandaliwa maandiko na watu wengine kwa gharama kubwa  na  bila kuwafafanulia yaliyomo ndani ya andiko la mradi". Amesema Mhe. Tegamaisho.

Katika utoaji wa Mikopo itolewayo na Halmashauri  kutoka mapato ya ndani kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kwa awamu ya kwanza Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ilitenga shilingi bilioni moja na ilipokea maombi ya vikundi 460 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.7 na vikundi vilivyokaguliwa kwa awamu ya kwanza ni 158, vilivyotimiza vigezo vya kupata mkopo ni vikundi 98  ambapo vimepatiwa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 764.5.

Akiwasilisha taarifa mbele ya Baraza Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Bi. Beatrice Sanga amesema Vikundi 13 vilipata changamoto ya kupokea fedha kutokana na BOT kushindwa kuingiza fedha kutokana na baadhi ya akaunti kutohuishwa na kutofautiana kwa majina ya vikundi kwenye mfumo wa usajili na majina ya akaunti zao za benki.

"Mpaka sasa tumefanya ufuatiliaji na vikundi 10 kati ya 13 havijapokea mkopo na tuandelea kufanya ufuatiliaji hivyo wawe na subira". Amesema Bi. Sanga

Ameongezea kwamba vikundi vitakavyo kaguliwa kwa awamu ya pili ni 286 na tayari Mkurugenzi Mtendaji ameshatangaza uwepo wa shilingi bilioni 1.6 kwa dirisha la pili kwa vikundi vitakavyokidhi vigezo.

Kwa upande wa madeni ya mikopo iliotolewa kipindi cha nyuma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi amepokea maelekezo ya Baraza juu ya kukusanya deni la shilingi milioni 289.5 kutoka vikundi 63 ili ziweze kukopeshwa kwa watu wengine.

Baraza hilo la siku mbili lilipokea na kujadili taarifa za utekelezaji za kata  zote 20 za Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa siku ya kwanza na siku ya pili limepokea na kujadili taarifa za utekelezaji za kamati za kudumu za Halmashauri.


Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa