• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Uviko19
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

MIKOPO: MILIONI 526.7 ZATOLEWA KWA VIKUNDI VYA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU

Posted on: February 10th, 2023

Leo tarehe 10 Februari 2023 Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi limeidhinisha mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani yenye thamani ya shilingi milioni 526.7 kwa vikundi vya vijana 22, wanawake 42 na 04 vya watu wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa utoaji wa mikopo hio mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. Projestus Tegamaisho alisema kwamba mpaka sasa kajawa na vikundi vyenye uwezo mkubwa wa kuchukua angalau milioni 50 na wakafanya ujasiriamali na vikundi vya namba hii tunavihitaji laki bado havijapatikana wakati halmashauri ina uwezo wa kutoa fedha hizo.

"Kila wakifanya ukaguzi wanasema hali walioikuta inafanana na kiasi cha fedha mlizopewa sasa tunataka vikundi vinavyoweza kuchukua fedha nyingi" Alisema Bw. Tegamaisho

Aidha alisisriza kwamba baraza la Madiwani wamekubalia kwamba hii itakua mara ya mwisho kugawa pikipiki kwani vijana walio wengi wanaishia barabarani hali inayosababisha kupoteza vijana wengi kwenye ajali na wengine kukimbilia huko kwakuona ndio shughuli nyepesi ya kufanya.

"Tumejipanga kama baraza la madiwani kuhakikisha wilaya yetu inaingia katika kilimo cha Parachichi aina ya HASS na Mibuni ili tuweze kuingiza kipato cha kutosha kwa kuhakikisha tunagawa miche kila kaya bure na wataalamu wa kutoa elimu" alisema Bw. Tegamaisho.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. Waziri Khachi Kombo alisema tutaendelea kukusanya mapato kwa hali na mali ili kuhakikisha fedha za mikopo zinapatikana kwa wingi zaidi ya hii iliyotolewa.

"Nitoe rai kwa wenye sifa za kukopa wachangamkie fursa hii haswa kwa kuweka vitega uchumi vinavyoeleweka na vitakavyorudisha fedha waliyopewa na serikali". Alisema Bw. Kombo.

Akitoa taarifa ķatika baraza la madiwani Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bi. Beatrice Sanga alisema idadi ya vikundi vilivyo omba mkopo katika robo hii ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23 vilikua vikundi 86 ambapo vikundi na vilivyokidhi vigezo ni 68 na vikundi 18 vilipoteza sifa.

"Sababu za kukosa sifa ni pamoja na Baadhi ya wanachama kuzidi umri haswa kwa vijana ambao wanapaswa kuwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 35, baadhi ya vikundi kuwa na wanachama pungufu ya watano na baadhi yao kutofautiana sana wakayi wa mahojiano hali inayotupelekea kugundua kwamba mradi sio wa kikundi bali ni wa mtu mmoja au wawli” Alimema Bi. Sanga.

Ikumbukwe kwamba mikopo hii inayotolewa kutokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri haina riba wala gharama ya namna yeyote na kiasi utakachopokea ndicho unachopaswa kurudisha na si vinginevyo.

.



Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2023 March 06, 2023
  • WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWAPELEKA WATOTO SHULENI January 07, 2023
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • TANGAZO LA UCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA 2023 March 02, 2023
  • Tazama zote

Habari mpya

  • USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI WABORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA SHULENI

    March 10, 2023
  • DC MISSENYI : NAWAAGIZA VYOMBO VYA DOLA KUHAKIKISHA MNAZUIA UKATILI WA KIJINSIA.

    March 08, 2023
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA MISSENYI KATIKA KATA ZOTE 20

    March 07, 2023
  • ZIARA YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI KATIKA WILAYA YA KYERWA

    February 16, 2023
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • JINSI YA KUOMBA MKOPO KUTOKA BODI YA MKOPO
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa