• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Uviko19
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

ZIARA YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI KATIKA WILAYA YA KYERWA

Posted on: February 16th, 2023

Leo tarehe 15 Februari 2023 baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi limefanya ziara katika Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa kwa ajili ya kujifunza namna walivyofanikiwa katika ukusanyaji wa mapato kupitia zao la kahawa ambalo kwa Wilaya ya Kyerwa limekua chanzo kikubwa kinacho ongoza kwa kuingizia Halmashari ya Kyerwa mapato mengi.

Baraza hili la madiwani Missenyi limeadhimia kuongeza mapato yatokanayo na kahawa kwani kwa mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri ya wilaya ya Missenyi ilikusanya shilingi milioni 145 ukilinganisha na Kyerwa amabayo imekusanya shilingi Bilioni 2 na ndio maana baraza likaamua kwenda katika Wilaya jirani kujifunza na kuona sababu zinazopelekea kupata mapato makubwa kupitia zao hili.

Hata hivyo kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Kyerwa kupitia zao la kahawa walipanga kukusanya shilingi Bilioni 1.2 lakini mpaka sasa wameshavuka lengo kwa kukusanya kwa asilimia 175 ambapo washakusanya shilingi bilioni 2.1 kwa chanzo hiki kimoja cha zao la kahawa.

Moja ya sababu ya kijiografia ambapo ilibainika katika ziara hii ni kwamba katika Wilaya ya Kyerwa wana eneo linalofaa kwa kilimo lipatalo hekta 26,000 wakati Missenyi ni Hekta 6,000 ambapo eneo la wilaya ya missenyi ni tambarare na linatuama maji ukilinganisha na Kyerwa ambapo kuna miinuko ya milima na mabonde.

Hata hivyo tija ya mti mmoja katika Wilaya ya Kyerwa una uzalishaji wa Wastani wa mti kwa kahawa ya maganda ni kilo 2.1 kwa Kyerwa wakati Missenyi ni Kilo 0.8 na hali hii imetokana na usambazaji wa miche bora iliosambazwa kwa wakulima, utunzaji mzuri Pamoja na udhibiti wa utoroshwaji wa kahawa kipindi cha mavuno.

ongeazeko la bei ya kahawa katika Wilaya ya Kyerwa ni jambo lililobainishwa na afisa kilimo wa Halmashauri hio kwa kwani kwa mwaka wa fedha uliopita 

Akizungumza katika ziara hio Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mhe. Projestus Tegamaisho aliwapongeza Kyerwa kwa kuhakikisha kwamba Kahawa haisafirishwi nje ya Kyerwa kwa ajili ya kwenda kukobolewa ambapo kwa usimamizi wao mzuri wamefanikiwa kupata wawekezaji waliofungua viwanda vinne mpaka sasa na kahawa yao inakobolewa ndani ya Wilaya yao halik inayokongeza thamani, tija na ajira khwa wananchi wa Kyerwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico Lekayo alisema nawapongeza Halmashauri ya Missenyi kwa kufanya ziara katika Wilaya yao kwani ni mara ya kwanza kupokea waheshimiwa madiwani kutoka wilaya nyingine kwa ajili ya kuja kujifunza kwao na inatia Faraja sana katika mustakabali wa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.

Mafanikio ya Wilaya ya Kyerwa katika zao hili la Kahawa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hio Mwl. Ndabazi Stephano Paulo alisema uchaguzi wa Miche bora na kinzani na magonjwa ya kahawa ni swala la muhimu sana na sio kuotesha tuu na jambo hili limesaidia sana katika kuongeza uzalishaji, aidha uzalishaji mkubwa wa miche bora wanaoufanya pamoja na ugawaji wa miche hio kwa wanachi wa halmashauri yao ambapo 2020/2021 miche 1,080,285 na kwa mwaka 2021/2022 waligawa miche 3,724,717 na kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 wanatarijia kugawa miche takribani milioni 2 kwa wakulima wa Kyerwa na miche mingine wanatarajia kugawia halmashauri jirani ili kuongeza uzalishaji katika taifa kwa ujumla.


Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2023 March 06, 2023
  • WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWAPELEKA WATOTO SHULENI January 07, 2023
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • TANGAZO LA UCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA 2023 March 02, 2023
  • Tazama zote

Habari mpya

  • USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI WABORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA SHULENI

    March 10, 2023
  • DC MISSENYI : NAWAAGIZA VYOMBO VYA DOLA KUHAKIKISHA MNAZUIA UKATILI WA KIJINSIA.

    March 08, 2023
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA MISSENYI KATIKA KATA ZOTE 20

    March 07, 2023
  • ZIARA YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI KATIKA WILAYA YA KYERWA

    February 16, 2023
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • JINSI YA KUOMBA MKOPO KUTOKA BODI YA MKOPO
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa