• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WAZEE WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUDUMISHA AMANI NA KUHIMIZA MALEZI BORA KWA VIJANA

Posted on: October 1st, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amewataka Wazee Wilayani humo kuwa chachu ya kudumisha amani na kuhimiza malezi bora kwa Vijana.

Hayo ameyasema leo Oktoba 01, 2025 katika Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani ambapo Kiwilaya maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Minziro iliyopo Kata ya Minziro.

"Kama mnavyofahamu, amani na usalama ni msingi wa maendeleo, bila ya amani hakuna maendeleo; na zaidi, pasipo na amani, wenye kuathirika zaidi ni pamoja na Wazee. Hivyo ni waombe muwe mabalozi wazuri wakudumisha amani", amesema Mhe. Maiga.

Ameongezea kuwa Wazee hawana budi kuhimiza malezi bora kwa Vijana ili kuendelea kujenga Taifa lenye uadilifu.

"Mimi naamini, Vijana wetu wakilelewa vizuri tutajenge Taifa la watu waadilifu, waaminifu na wazalendo kwa nchi yao, wasiojihusisha na vitendo viovu vya wizi, rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine ambavyo ni kinyume cha maadili na tamaduni zetu. Hivyo Wazee hamna budi kuendelea kuhimiza malezi bora kwa Vijana wetu", ameongezea Mhe. Maiga.

Awali akisoma risala ya Wazee wa Wilaya ya Missenyi, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Wilaya ya Missenyi, Mzee Lenatus Leo, amesema kuwa, wao kama Wazee wanaomba kutimiziwa baadhi ya mambo ili kuweza kukidhi matibabu ya wazee na kujikwamua kiuchumi.

"Sisi Wazee wa Wilaya ya Missenyi kwa pamoja tunaomba, Vitambulisho vya Wazee vipandishwe hadhi ili kuweza kukidhi matibabu kwa Wazee, zoezi la vitambulisho kwa Wazee liwe endelevu, tupewe mikopo kwa riba nafuu, na tupate wawakilishi ngazi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kila Wilaya", amewasilisha Mzee Lenatus.

Aidha, amesisitiza kwamba Wazee ni miongoni mwa makundi maalumu amabayo yanahitaji kutazamwa kwa jicho la pekee kama makundi mengine.

Maadhimisho haya ya Siku ya Wazee Duniani hufanyika Oktoba 01 kila mwaka, ambapo kwa Tanzania kwa mwaka huu maadhimisho haya yameambatana na kauli mbiu isemayo; " Wazee tushiriki Uchaguzi kwa Ustawi wa Jamii yetu".

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WAZEE WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUDUMISHA AMANI NA KUHIMIZA MALEZI BORA KWA VIJANA

    October 01, 2025
  • HALMASHAURI YAWAKUTANISHA WADAIU WA KILIMO NA TAASISI ZA KIFEDHA

    September 24, 2025
  • WAKAZI 7,562 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MUTUKULA

    September 10, 2025
  • WAJAWAZITO WATAKIWA KUTUMIA KWA WAKATI DAWA ZA KUONGEZA DAMU

    September 04, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa