• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

TFS MISSENYI YAKABIDHI MADAWATI 90 KWA SHULE ZA SEKONDARI BUNAZI NA MUTUKULA

Posted on: March 7th, 2025

Leo tarehe 07/03/2025 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekabidhi madawati 90 kwa Shule za Sekondari Bunazi na Mutukula.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kilichopo Kata ya Gera Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi ambaye pia ni Kamanda wa TFS Kanda ya Ziwa Ebrantino E. Mgiye amesema TFS itaendelea kushirikiana na taasisi za serikali kuhakikisha wanendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia.

"TFS tutaendelea kushirikiana na taasisi za serikali ikiwepo shule kuhakikisha kwamba tutaendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia, tunafahamu kwamba kadri mazingira sahihi ya kujifunza yanavyopatikana na wanafunzi wanapata elimu ambayo ni sahihi kabisa". Amesema Ebrantino Mgiye.

Kwa upande wake Mhifadhi Misitu Wilaya ya Missenyi kutoka TFS Bw. Mrisho Juma akisoma taaarifa fupi wakati wa makabidhiano hayo amesema kwamba Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kutekeleza majukumu yake imekuwa ikitoa michango inayoigusa jamii katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu.

Aidha amesema kwamba TFS Wilaya ya Missenyi kwa mwaka wa fedha 2024/25 iliweka lengo la kutoa madawati 90 kwa shule za Sekondari za Bunazi na Mutukula ambapo leo hii madawati hayo yamekabidhiwa na mradi huo wa madawati 90 pamoja na viti 90 umegharimu Shilingi Milioni 5.9 ikiwa ni fedha ya vyanzo vya ndani vya taasisi.

Akipokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amewashukuru TFS kwa kuendelea kuigusa jamii ya Wana Missenyi hususani katika sekta ya elimu kwa kuchangia Madawati 90 kwa Shule za Sekondari Bunazi na Mutukula.

"Siku zote TFS Wilaya ya Missenyi wamekuwa wakitengeneza kila mwaka madawati 45 mpaka 50, lakini tuliona ile idadi ni ndogo tukaweka kilio chetu na kilio kimesikilizwa na leo tumetoka 45 tuko 90, kwahiyo muendelee na moyo huo huo wa kujitoa". Amesema Mhe. Hamis Maiga.

Aidha amewataka Walimu wa shule zilizopewa madawati hayo kuhakikisha zinayatunza vizuri kwani amekuwa akipita kwenye baadhi ya shule na kukuta utunzaji wa madawati si mzuri.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Missenyi ambae pia amemuwakilusha Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. Dancras Ishengoma ameishukuru TFS kwa kuona umuhimu wa kutoa madawati hayo kwa wanafunzi kwani yataenda kupunguza idadi ya upungufu wa madawati kwa Shule za Sekondari Bunazi na Mutukula.

Pia ameongezea Kuwa watafuata na kutekeleza maelekezo waliyopewa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga juu utunzaji wa madawati hayo.

Madawati haya 90 yamegawanywa kwa Shule mbili za Sekondari Bunazi na Mutukula ambapo kila shule imepokea seti 45 za madawati yaani kiti na meza yake.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekuwa wakiigusa jamii katika nyanja mbalimbali na makabidhiano haya ya madawati 90 yatasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati katika Shule za Sekondari Bunazi na Mutukula, hivyo kuboresha mazingira ya kufundisha shuleni.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA MISSENYI

    May 16, 2025
  • WATENDAJI KATA NA VIJIJI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTOA ELIMU YA LISHE KWA JAMII

    May 14, 2025
  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa