• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

Posted on: June 26th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga ametoa wito kwa Viongozi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutokukubaliana na sera na masharti magumu ya Wafadhili yanayoweza kuwaingiza katika mgogoro wa Kisheria na kuhatarisha uhai wa Mashirika yao.

Mhe. Hamis Maiga ametoa wito huo leo Juni 26, 2025 katika Kongamano la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilayani Missenyi lenye lengo la kuelimishana juu ya masuala ya uendeshaji wa Mashirika hayo, ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ya utatuzi na kuwa na mpango endelevu wa kuimarisha utendaji wa Mashirika hayo.

Amesema kwamba Serikali haitosita kuchukua hatua kali endapo kuna Shirika lolote litakalotumia vibaya usajili wake kwa kujihusisha na vitendo viovu.

"Serikali ya Wilaya haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa Shirika lolote litakalotumia vibaya usajili wake kujihusisha na vitendo viovu vinavyokinzana na sheria, mila na desturi za nchi yetu", amesema Mhe. Maiga.

Aidha, ameongezea kuwa Serikali ya Wilaya ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuimarisha mahusiano na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kuiwezesha Wilaya ya Missenyi kusonga mbele.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo Bi. Tapita Tuvana ameyashukuru Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali.

"Napenda kutumia jukwaa hili kuzishukuru NGO's mnazowakilisha kwa namna zinavyoendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za wananchi na kunufaisha makundi mbalimbali kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta na nyanja mbalimbali", amesema Bi. Tapita.

Ameongezea kuwa mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ni Shilingi bilioni 5.1 Katika kipindi cha 2020/2021 hadi 2024/2025 ambapo fedha hizo zimetumika katika jamii kupitia mifumo ya utendaji wa Mashirika hayo kulingana na taratibu na mashariti ya ufadhili.

Hata hivyo, kupitia miradi hiyo fursa za ajira kwa vijana zimepatikana, uchumi wa jamii umeongezeka, uelewa na ari ya wananchi kujitolea imeongezeka pamoja na uhatarishi kwa makundi maalumu umepungua.

Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi na kuhudhuriwa na Viongozi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yaliyopo Wilayani Missenyi na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa