• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

Posted on: June 17th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat  Fatma Mwasa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.

Akizungumza katika Baraza maalum la Madiwani la Kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika katika Ukumbi wa William F. Katunzi uliopo Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi leo Juni 17, 2025, Mhe. Hajjat Fatma Mwasa amesema ana kila sababu ya kuipongeza Missenyi kwa kupata hati safi miaka 10 mfululizo.

"Nina kila sababu ya kuwapongeza kwa kupata hati safi kwa miaka 10 mfululizo, lakini sio tu kupata hati safi, mmepata hati safi kwa miaka 10 mfululizo mkiwa na hoja chache na zinazoelezeka, hii nayo imeleta faraja kubwa", amesema Mhe. Mwasa.

Aidha, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Mwenyekiti wa Halmashauri, Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji na Wataalamu wa Halmashauri kwa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja.

"Nimpongeze Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wetu na Wataalamu wetu, matunda yanayotokea Missenyi yanatokana na nguvu ya pamoja, yaani vile utendaji kazi mlionao, ushirikiano na kila kitu, hayo ndio yanayoleta matokeo chanya Missenyi", ameongezea Mhe. Mwasa.

Awali akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. John Paul Wanga amesema kwamba kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya ya Missenyi imepata hati safi.

Pia, amebainisha kwamba taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imejumuisha hoja za mwaka wa fedha 2023/2024, hali ya utekelezaji wa hoja za miaka ya nyuma kufikia mwaka wa fedha 2022/2023 pamoja na maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAC).

Ambapo amefafanua kuwa, katika mwaka wa fedha 2023/2024, hoja 15 ziliibuliwa na kutolewa mapendekezo, kati ya hoja ziliibuliwa na kutolewa mapendekezo, hoja 10 zimejibiwa kikamilifu na kufungwa na kusalia hoja 5 ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Kwa miaka ya nyuma hadi kufikia mwaka wa fedha 2022/2023, Halmashauri ilikuwa na hoja 17, kati ya hizo hoja 11 zimejibiwa kikamilifu na kufungwa na kusalia hoja 6 ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Ameongezea kuwa Halmashauri ilikuwa na maagizo matano kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAC), ambapo  hadi kufikia mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imefanyia kazi kikamilifu maagizo manne na kusalia na agizo moja ambalo lipo Katika hatua ya utekelezaji.

Aidha, kwa upande wa hoja za Miradi ya Afya, Elimu pamoja na Mfuko wa Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi amesema kwamba katika mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ilikuwa na hoja sita za Miradi ambapo hoja nne zimejibiwa kikamilifu na kufungwa na hoja mbili zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Akifunga Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mhe. Projestus Tegamaisho amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwasa kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchochea mafanikio katika Mkoa wa Kagera.

Aidha, amelieleza Baraza kwamba amehakikisha katika kipindi chake chote cha miaka 10 akiwa kama Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Halmashauri haipati hati chafu au hati yenye mashaka.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • WAZAZI WAHIMIZWA KUSHIRIKI KAMPENI YA UTOAJI WA MATONE YA VITAMINI A

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa