• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

HALMASHAURI YAWAKUTANISHA WADAIU WA KILIMO NA TAASISI ZA KIFEDHA

Posted on: September 24th, 2025


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. John Paul Wanga leo tarehe 24 Septemba 2024, amefungua Mkutano wa siku moja uliowakutanisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Taasisi za fedha kwa lengo la kuonyesha fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo zinazohitaji wakulima na taasisi za kifedha kuwekeza ili kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Halmashauri kwa ujumla.

Akizungumza na wadau wa kilimo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Bw. Wanga amesema kuwa lengo la kuwakutanisha kwa pamoja ni kuwaunganisha wakulima, wafanyabiashara, wafugaji, wavuvi na wadau wa taasisi za kifedha ili kuwaonesha fursa zilizopo kwenye wilaya kwa ajili kuwekeza kwenye fursa hizo.

“Ninawaomba mshiriki vyema na mtoe ushauri na mapendekezo yenu kwa taasisi za fedha ili wahamishe mawazo yao katika sekta ya kilimo na sio kwa watumishi na wamiliki wa maduka peke yao", amesema Bw. Wanga.

Kwa upande wake Afisa kilimo Bw. Subira John akibainisha fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo amesema  kwamba Missenyi ina eneo la kilomita za mraba 2708.75 ambapo takribani hekta 99,726 zinafaa kwa kilimo na kwa sasa karibu hekta 58,840 sawa na 59% ndizo zinazoendelezwa kwa kilimo licha ya kupata mvua mara mbili kwa mwaka kwa wastani wa 800-1,500 mm.

Aidha amebainisha kwamba uwepo wa Mito kama mto Kagera, Mto Ngono pamoja na mabonde, nyanda za chini, maeneo ya tambarare na mabwawa ya asili ni moja ya fursa katika sekta ya kilimo, uvuvi na Mifugo katika Wilaya yetu kwani huwezesha ufanyikaji wa kilimo cha umwagiliaji kwa urahisi.

Ameongezea kuwa bei ya ardhi bado ni rafiki ukilinganisha na maeneo mengine ambapo maeneo mengi katika wilaya ya Missenyi ni takribani shilingi 500,000/= hadi 1,000,000/= kwa ekari isiyoendelezwa hali inayoleta mazingira rafiki kwa anayehitaji kuwekeza.

‘’Fursa zinanzopatikana katika Halmmashauri ya Wilaya ya Missenyi ni pamoja na Uwekezaji kwenye mashamba makubwa ya kahawa aina ya Robusta, usindikaji na ufungashaji kwa ajili ya masoko ya kimataifa, Kilimo cha Miwa na nishati mbadala, Kilimo cha ndizi, Kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji kwa kutumia mabonde na tambarare, Kilimo cha mbegu bora za Nafaka, Kilimo cha bustani au mboga na matunda , uhifadhi na usindikaji wa mazao kama ndizi, mpunga na mahindi”, amesema Bw. Subira.

Kwa upande wake Bw. Labson Mwalusesa ambaye ni Afisa Mikopo kutoka benki ya CRDB amesema kwamba katika furza zilizowasilishwa katika mkutano wa leo bado zina kipaumbele cha kupata mikopo kutoka benki ya CRDB hususan katika eneo la kilimo ambapo mkulima anaweza kupata mkopo wa fedha Taslim kulingana na mazao anayolima na sio fedha Taslim pekee bali unaweza kukopeshwa zana za kilimo endapo utahitaji.

 Bw. Lasbon amesistiza kwamba benki ya CRDB ina fedha nyingi kwa ajili ya Sekta ya Kilimo, Mifugo na uvuvi ingawa bado wakulima hawajajua jinsi ya kutumia fursa hio.

 Kwa mujibu wa Bi. Lucia Musa ambaye ni Afsa mikopo wa benki ya NMB amesema kwamba benki yao inatoa mikopo mizuri kupitia sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa riba nafuu ya 16% hivyo wakulima wahakikishe wanatumia fursa hio ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wa wakulima, wafugaji na wavuvi waliohudhuria wamewasilisha changamoto zao wanazokumbana nazo hususan katika taasisi za kifadha ikiwa ni pamoja ukosefu wa hati kwani mashamba yao yanapatina maeneo ya ndani yasiofikika kiurahisi, milolongo mirefu kwenye taasisi za kifedha na kukosekana mrejesho, ubadilishwaji wa vigezo mara kwa mara bila sababu za msingi pamoja na kutumia fedha nyingi wakati wa kwenda na kurudi mara nyingi katika benki bila majibu ya kupata mkopo.

Mkutano huo umewakutanisha wadau wa kilimo na taasisi za kifedha umeandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilya ya missenyi kupitia divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.


Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WAZEE WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUDUMISHA AMANI NA KUHIMIZA MALEZI BORA KWA VIJANA

    October 01, 2025
  • HALMASHAURI YAWAKUTANISHA WADAIU WA KILIMO NA TAASISI ZA KIFEDHA

    September 24, 2025
  • WAKAZI 7,562 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MUTUKULA

    September 10, 2025
  • WAJAWAZITO WATAKIWA KUTUMIA KWA WAKATI DAWA ZA KUONGEZA DAMU

    September 04, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa