• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA KAGERA KATIKA WILAYA YA MISSENYI

Posted on: February 2nd, 2023

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Albert Chalamila amefanya ziara ya siku tatu katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi na kufanya mikutano ya hadhara.

Akiwa Wilaya ya Missenyi Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ametembelea tarafa mbili za Wilaya ya Missenyi ambazo ni Kiziba na Missenyi ambapo terehe 31/01/2022 atakua tarafa ya Kiziba na tarehe 02 na 03/02/ 2022 atakua tarafa Missenyi katika Kata za Kakunyu, Kassambya na Kyaka.

Katika tarafa ya kiziba miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule ya sekondari Kitobo, Mradi wa maji Buyango pamoja na kufanya mikutano ya hadhara katika shule ya sekondari Kitobo, Mradi wa Maji Buyango na Uwanja wa Shule ya Msingi Mugana B.

Aidha katika tarafa ya Missenyi katika kata ya kakunyu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara, ametembelea na kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Kakunyu, ametembelea barabara ya TARURA ya Kakunyu - Bugango yenye urefu wa kilomita 12.5 na Barabara ya TARURA ya Missenyi Ranch - Bugango yenye urefu wa kilomota 12 pamoja kutembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Uganda katika kata ya Kakunyu katika eneo maarufu kama jiwe namba 27.

Hata hivyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa atahitimisha ziara yake katika kata ya Kassambya na Kyaka kwa kutembelea Kiwanda cha Kukoboa kahawa cha Muwekezaji SOURCE OF NILE COMMODITIES, kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Kagera na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika stendi ya Kyaka na kufanya mkutano wa hadhara katika stendi ya Kyaka.

Wakati akiweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Kitobo inayojengwa kama shule ya mfano kupitia serikali kuu ambapo mpaka sasa serikali kuu imeshatoa jumla ya shilingi milioni 470 na Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetoa shilingi milioni 100 ameishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi katika mkoa wetu wa Kagera zinazojenga miundo mbinu mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji na barabara bila kuwachangisha wananchi hali ambayo imeondoa adha ya michango mbalimbali ya mara kwa mara kwa wananchi.

Aidha aliwapongeze wananchi wa kitobo kwa ujumla kwa kukubaliana na kutoa ardhi hii ili tujenge Shule hii inayokwenda kusaidia vizazi na vizazi kwani maeneo mengine badala ya kutoa ardhi wanaishia kwenye malumbano yasiokua na tija.

" Jukumu lenu wazazi ni kuhakikisha wanaitunza miundo mbinu, wahakikishe watoto wanafika shule kwani miundo mbinu hii iliyowekwa hapa ni kwa ajili ya watoto wetu na wanafunzi wahakikishe wanajukumu moja tuu la kusoma kwa bidii na wajiepushe na vitendo viovu haswa mahusiano ya kimapenzi." Alisema Bw. Chalamila.

Alisisitiza kwamba hatawafumbia macho viongozi wanaoshiriki kuhujumu watoto kupata haki yao ya elimu kwani kumekua na ndoa zinazojitokeza kwa watoto wanaopaswa kuripoti shuleni na vingozi haswa wenyeviti wa vijiji madiwani na watendaji wanafahamu na hawatoi taarifa wala ushirikiano.

Aliwasihi wanachi kuhakikisha wanaitunza miundo mbinu ya shule kwa ni mali yao pamoja na kuwasihi vijana ambao wameshapata elimu kuhakikisha wanazitumia elimu zao kuisadia jamii badala ya kulalamika juu ya ajira.

Ujenzi wa shule ya sekondariya Kitobo unajumuisha Ujenzi wa madarasa 8 na Ofisi ndogo 4 za Walimu ambao umefikia 99%, Ujenzi wa maabara ya Physics, Biology na Chemistry umefikia 99%, Ujenzi wa jengo la Utawala umefikia 99%, Ujenzi wa Choo cha Matundu 10 Wasichana na Matundu 10 ya Wavulana uliokamilika 100%, Ujenzi wa jengo la ICT umefikia 90% na Ujenzi wa jengo la Maktaba 97%.

Mhe. Mkuu wa Mkoa alitembelea mradi wa maji uliopo chini ya Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA katika kata ya Buyango wenye thamani ya shilingi milioni 792.3 uliojengwa kwa vyanzo vya fedha zitonanazo na UVIKO-19 na PforR.

Akizungumza na wananchi baada ya kukagua mradi Mhe. Chalamila alisema ili kuacha alama Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan aliamua kujenga mradi huu ila wananchi wapate maji safi na salama ya kunawia na kuweza kujitakasa.

Kwa upande wake Mheshimiwa diwani wa kata ya buyango Bi. Regina Ramuganga ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Missenyi amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kufanya kata ya Buyango kuwa miongoni mwa maeneo yaliopata kipaumbele cha kupewa mradi huu wa maji.

Akitoa taarifa ya mradi Mhandisi Andrew Kilembe amesema mpaka sasa kaya 118 wameunganishiwa maji majumbani, Taasisi nne (4) ambazo ni Shule ya Msingi Buyango, Shule ya Msingi Omukajuju, Shule ya Sekondari Buyango, Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri (KKKT) Buyango wanapata huduma ya maji safi na zoezi la kuunganisha maji majumbani ni endelevu.

Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 21 Januari 2022 na kukamilika tarehe 22 Juni 2022 kupitia mkandarasi Advanced Engineering Co.Ltd na umelenga kuwadumia wananchi wapatao 3,912 katika vijiji vya Rwamachu, Rutunga na Vijiji jirani na Vilevile ukamilishaji wa usambazaji wa maji awamu ya pili kwa vijiji vya Kishoju, Kikono na Rushasha unaendelea.

Katika kuhitimisha ziara yake katika tarafa ya kiziba kwa kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Bwanjai katika uwanja wa shule ya msingi Mugana B, Mkutano uliwapatia wananchi fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa na kuapata majibu kutoka kwake na wataalamu mbalimbali alioambatana nao katika ziara yake.

Maswala yalioulizwa na wananchi walio wengi ni pamoja na kusogezwa kwa huduma ya Maji, umeme, vitambulisho vya NIDA, Matumizi ya mbolea ya ruzuku,Barabara kuwekewa lami, usalama barabarani, uhamiaji, maswala ya elimu na Afya.

Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa