• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WALIOVAMIA MSITU WA BUSHENYA WATAKIWA KUONDOKA IFIKAPO MACHI 30, 2025

Posted on: February 14th, 2025

Wananchi waliovamia msitu wa Bushenya Wilayani Missenyi wametakiwa kuhakikisha wanavuna mazao yao na kuondoka katika msitu huo mpaka kufikia tarehe 30/03/2025.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Februari 14, 2025 katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amebainisha kwamba kwa mipango iliyowekwa kwasasa watakapowaondosha wananchi hao waliovamia eneo la msitu hawatarudi tena katika eneo hilo.

"Kwa historia ya hili jambo oparesheni nyingi zimefanyika pale na hazina mafanikio, nataka niwahakikishie tulivyojipanga mara hii tutakapowaondosha hawatarudi, kwasababu uondoshaji wa mwaka huu umeangalia mapungufu yaliyotokea kwenye uondoshaji wa miaka ya nyuma". Amesema Kanali (Mst) Hamis Maiga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya ya Missenyi Bw. John Paul Wanga amesema kwamba wananchi waliopo katika msitu wa Bushenya hawatambuliki kwa mujibu wa sheria.

"Wananchi walioko kule ndani ya msitu hawatambuliki na sheria zetu za Serikali za mitaa, kwasababu ili utambulike lazima Kijiji kianzishwe kwa mujibu wa sheria na Mheshimiwa Rais hajaanzisha Kijiji cha Bushenya". Amesema Bw. John Wanga.

Aidha ameongeza kuwa Wananchi wanaolalamika ni wavamizi na wanatakiwa kuondoka katika msitu huo na eneo hilo litatumika kwa shughuli rasmi za mazoezi ya kijeshi na hawatagusa vijiji vilivyopo jirani na eneo hilo bali watajihusisha na eneo la hekta 9000 tu.

Kutokana na uvamizi wa wananchi katika msitu huo, mpaka sasa eneo lililovamiwa ni wastani wa hekta 4000 ambapo hekta 5000 zimeonekana hazina tatizo na uvamizi huo umepelekea kutoweka kwa viumbe na mimea mbalimbali ya porini, uharibifu wa misitu, kukauka na kupungua kwa vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa madogo ya Kayanja na Byeju.

Mkutano huo na Waandishi wa Habari ulihudhuriwa pia na Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji vinavyopakana na msitu huo wa Bushenya unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa