• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

Posted on: April 25th, 2025

Leo Aprili 25, 2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imefanya kikao na wadau wa uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kujiridhisha kuwa utaratibu wa kubadili jina la Jimbo la uchaguzi kutoka Nkenge na kuwa Missenyi umefuatwa.

Akizungumza katika Kikao hicho cha kupitia maombi ya kubadili jina la Jimbo la uchaguzi la Nkenge, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk amesema kwamba kwa mujibu wa kanuni ya 18 ya kanuni za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024, Tume imechagua kutembelea majimbo yote yalioomba kubadilisha jina kwa lengo ya kujiridhisha iwapo taarifa hizo zilizopo kwenye maombi yaliyowasilishwa ni sahihi kuhusu jimbo husika.

Aidha, amewapongeza wajumbe katika Kikao hicho kwa kukubaliana kwa kauli moja kuwa maombi yaliyowasilishwa ni sahihi na yalifuata utaratibu.

"Nawapongeza kwa kuifanya kazi yetu kuwa nyepesi na kwa kauli moja mmekubaliana kuwa maombi yaliyowasilishwa ya pendekezo la kubadili jina la Jimbo la Nkenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera ni sahihi kwa mujibu wa barua iliyowasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa". Amesema Mhe. Mbarouk.

Pia amesisitiza kuwa kufanyika kwa kikao hicho haina maana kuwa ombi la kubadili jina la Jimbo la uchaguzi limekubaliwa.

"Tunawasihi kwamba kikao hiki haina maana kuwa sasa ombi lenu limekubaliwa bali Tume huru ya Uchaguzi imetimiza matakwa ya kanuni ya 18 ya kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024 za kutembelea majimbo yaliyoomba kubadilisha jina la Jimbo, hivyo Tume itakutana na kuendelea kuchakata taarifa zote na baada ya hapo kwa kuzingatia mashariti ya Katiba na Sheria itatangaza majimbo yaliyogawanywa na yaliyobadilishiwa majina". Amesema Mhe. Mbarouk.

Kikao hicho baina ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kilikuwa na lengo la kujiridhisha kama utaratibu wa vikao vilivyopangwa Kisheria kwa maana ya kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) na Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) vilikaa na kupendekeza maombi hayo.

Hata hivyo, Wajumbe katika Kikao hicho wamethibitisha kuwa vikao hivyo vilifanyika na kwa kauli moja wamekili kuwa maombi ya kubadili jina la Jimbo la Nkenge ni sahihi.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA MISSENYI

    May 16, 2025
  • WATENDAJI KATA NA VIJIJI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTOA ELIMU YA LISHE KWA JAMII

    May 14, 2025
  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa