• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

RC SHIGELA AFANYA ZIARA KATIKA MPAKA WA MUTUKULA.

Posted on: June 28th, 2023

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela leo tarehe 28 June, 2023 amefanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Missenyi.


Akiwa Missenyi ametembelea kituo cha pamoja cha forodha cha Mutukula, amekagua eneo la mpaka kati ya Tanzania na Nchi ya Uganda , amezungumza na watumishi wa kituo hicho   pamoja na kufanya mkutano na wafanyabiashara wa Wilaya ya Missenyi hususan wanaotumia mpaka wa Mutukula kusafirisha Mazao na bidhaa mbalimbali.


Akizungumzia juu ya sheria ndogo ya Halmashauri ambapo wafanyabiashara waliataka kupata ufafanuzi juu ya uwepo wa sheria ya usafirishaji na upitishaji wa mazao katika Wilaya ya Missenyi aliwataka wafanyabiashara wote wanaotumia mpaka wa Mutukula kuwa wavumilivu na kuendela kufuata utaratibu wa ulipaji wa Ushuru kwa mujibu wa sheria ndogo ya Halmashauri iliyopo sasa.


 Aidha aliagiza Ngazi ya Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi,Uongozi wa Mkoa na Wafanyabiashara kupitia sheria ndogo ya Halmashauri inayohusiana na usafirishaji wa mazao ili kuweka makubaliano juu ya namna bora ya ukusanyaji wa tozo kupitia biashara ya Mazao.

“Nimefarijika sana kuona wafanyabiashara wa Wilaya ya Missenyi wako tayari kulipa kodi hivyo niwakumbushe kwamba Halmashauri haitaweza kujiendesha na kutoa huduma kwa wananchi endapo ushuru hautalipwa, hivyo ni vyema ukawekwa utaratibu ambao Halmashauri itapata mapato na wananchi wakafanya biashara bila kuwa na kikwazo chochote" Alisema Mhe. Shigela


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ndg. Toba Nguvila ameeleza kuwa kutokana na agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuruhusu mazao kuendelea kusafirishwa nje ya Nchi kwa masharti ya mfanyabiashara awe amekidhi vigezo pamoja na kufuata taratibu zote za ikiwa ni pamoja na vibali  vinavyotakiwa.


"Sisi kama uongozi tumefika mpakani hapo ili kuona shughuli za kiutendaji na kupokea changamoto za wafanyabiashara zinazotokana na agizo hilo" Alisema Bw. Nguvila.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Missenyi, Bw. Sakibu Seleman ameeleza kwamba wao wanaomba waendelee kulipia ushuru wa mazao kwa gari kama ilivyokua kipindi cha nyuma na sio kwa gunia ilivyo sasa ambapo kila gunia moja walikua wanlinalipa tshs 1,600/- wakati ukilipa kwa gari zinazojulikana kwa majina maarufu ya aina ya Semi ilikua tshs 140,000/-,  Tandam 90,000/- na Fuso ilikua tshs 60,000/- ambapo ukilipa kwa gunia inakua gharama sana.


Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi akitoa ufafanuzi juu utozaji wa ushuru wa mazoa Bw. Dotto Mayombo alisema kwa mujibu wa sheria ndogo za Halmashauri ya mwaka 2019/2020 imebainisha wazi kwamba kila gunia la kilo 100 litatozwa tshs 2,000 ingawa kwa sasa tunatoza tshs 1,600/- kwa kila gunia na tunarajia kuanzia mwaka wa fedha utakaoanzia 01 July 2023 tutaanza kutoza tshs 2,000 kama sheria inavyoelekeza.



Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa