• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

MRADI WA LISHE SHULENI WAZINDULIWA MISSENYI

Posted on: July 22nd, 2025

Leo Julai 22, 2025 Shirika la Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) limetambulisha mradi wa Lishe shuleni (Lishe Shuleni Project) kwa Wilaya ya Missenyi wenye lengo la kuimarisha hali ya lishe katika Shule za Msingi na Sekondari Wilayani humo.

Utambulisho huo umeenda samabamba na uzinduzi wa mradi ambapo Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Hamis Maiga ameuzindua mradi huo, na kuanza kufanya kazi rasmi kwa Wilaya ya Missenyi.

Akizungumza katika utambulisho na uzinduzi wa mradi huo Meneja Mradi wa urutubishaji chakula kutoka GAIN Bw. Archard Ngemela amesema kwamba mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Kagera ambazo ni Muleba, Bukoba Vijijini na Missenyi.

Ameongezea kuwa mradi huo unalenga kufanya kazi na Shule pamoja na jamii ili kuweza kuzalisha vyakula vilivyorutubishwa kibaiolijia.

Aidha, amesema kuwa wamelenga kufanya kazi na Kata sita kila Halmashauri, ambapo kila Kata itatoa Shule moja ya Sekondari na mbili za msingi ili kushiriki katika mpango huo, hivyo katika kila Halmashauri watafanya kazi na Shule za Msingi 12 na Sekondari sita.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bi. Tapita Tuvana amesema kwamba vigezo vilivyotumika kupata Shule zitakazokwenda kuwakilisha mpango huo ni pamoja na wingi wa  Wanafunzi katika Shule hizo, Upatikanaji wa maeneo ya kilimo katika Shule husika lakini pia kuangalia Shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu pamoja na hali ya lishe katika Shule husika.

Aidha, amebainisha Kata na Shule zitakazoshiriki katika mradi huo kwa Wilaya ya Missenyi ambapo amesema katika Kata ya Kakunyu, Shule za Msingi Bubale na Bwenkoma pamoja na Shule ya Sekondari Kakunyu zitashiriki.

Kata ya Nsunga Shule za Msingi Omulungando na Byamutemba pamoja na Shule ya Sekondari Nsunga zitashiriki. Hivyo hivyo, katika Kata ya Kassambya Shule za Msingi Bunazi 'B' na Gabulanga pamoja na Shule ya Sekondari Gabulanga zitashiriki.

Kwa upande wa Kata ya Kyaka Shule za Msingi Kyaka na Kimkunda pamoja na Shule ya Sekondari Kagera zitashiriki, ambapo kwa Kata ya Kilimilile Shule za Msingi Mwemage na Mabale pamoja na Shule ya Sekondari Kilimilile zitashiriki pia.

Tarafa ya Kiziba imetoa Kata moja ya Kitobo ambapo Shule za Msingi Mbale na Kayanga pamoja na Shule ya Sekondari Bwabuki zitashiriki katika mradi huo.

Mradi huu utatekelezwa kwa muda wa miezi 12 ambapo Shule hizo zitawezeshwa kupata mbegu za maharage lishe, mahindi lishe na viazi lishe ili ziweze kulima katika maeneo ya Shule na washirikiane na Maafisa Kilimo wa maeneo husika, vile vile sehemu ya mpango huu inarudi kwa jamii husika ambapo zenyewe zitapewa mbegu na Wataalamu wanaopatikana kwenye Kata ili waweze kuzalisha chakula kilichorutubushwa.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MRADI WA LISHE SHULENI WAZINDULIWA MISSENYI

    July 22, 2025
  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa