• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Uviko19
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

MRADI MPYA WA BOOST KUJENGA VYUMBA 12,000 VYA MADARASA

Posted on: December 22nd, 2022

Mafunzo Elekezi kuhusu Mradi wa BOOST yanayofanyika kikanda yameanza leo tarehe 22 Disemba 2022 katika kanda ya Ziwa Magharibi inayojumuisha Mkoa wa Kagera na Kigoma ambapo jumla ya Maafisa 207 kutoka ngazi ya Halmashauri na Mikoa wanatarajiwa kupata mafunzo haya katika kanda hii.

Mafunzo haya yalioandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na yatafanyika kwa siku mbili katika Mkoa wa Kigoma katika chuo cha Ualimu cha KASULU kilichopo katika Wilaya ya Kasulu.

Mradi wa BOOST utagharimu shilingi Trilioni 1.15 kwa nchi nzima na unalenga kujenga jumla ya vyumba vipya vya madarasa 12,000 katika shule za msingi na kuwesha kutekeleza mpango wa shule salama katika shule za msingi 6,000 hapa nchini.

Mradi unatekelezwa hapa nchini kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2025/2026 na kunufaisha halmashauri zote 184 hapa nchini hususani katika kuboresha miundombinu ya elimu ya Awali na Elimu Msingi.

Aidha Mradi wa BOOST unatarajiwa kuboresha mazingira ya ujifunzaji na Ufundishaji, Ujuzi na Ubora wa walimu katika ufundishaji, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za utoaji huduma za elimu ngazi ya Halmashauri Pamoja na kuongeza uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali kutoka asilimia 76.9 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2025/2026.

Ikumbukwe kwamba mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa lipa kutokana na matokeo yanayopatikana hivyo Halmashauri ambazo zitatimiza vigezo kwa kiwango kikubwa ndizo zitakazonufaika zaidi kwa kupatiwa fedha nyingi za kuboresha miundombinu pamoja na ununuzi wa vifaa na vitendea kazi kwa elimu ya Awali na Msingi.

Wajumbe wa timu za usimamizi wa mradi wa BOOST ngazi ya Halmashauri inajumuisha Afisa Elimu Msingi, Afisa Maendeleo ya Jamii, Mhandisi, Mwalimu Mkuu, Afisa Manunuzi, Mthibiti Ubora wa Shule, Afisa Ustawi wa Jamii, Afisa Elimu Kata, Afisa Mipango, Afisa Habari na Mratibu wa Mradi wa BOOST na ngazi ya Mkoa inaundwa na Afisa Elimu Mkoa, Mratibu wa Mradi wa BOOST, Mhandisi, Afisa Habari, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Ustawi wa Jamii, Afisa Mipango na Mthibiti Ubora wa Shule Kanda.


Tarifa Kwa Umma

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera Region August 19, 2022
  • TAHADHARI YA EBOLA October 02, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA SEKONDARI October 05, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI TAREHE 08/11/2022. November 03, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.3 KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2022/23ROBO YA

    January 20, 2023
  • MRADI MPYA WA BOOST KUJENGA VYUMBA 12,000 VYA MADARASA

    December 22, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU

    December 09, 2022
  • MISSENYI DC: UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA UMEFIKIA ASILIMIA 98%

    November 27, 2022
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • JINSI YA KUOMBA MKOPO KUTOKA BODI YA MKOPO
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa