• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.6 IMEKAGULIWA NA MWENGE WA UHURU 2023 WILAYA YA MISSENYI.

Posted on: August 11th, 2023

Leo tarehe 11 Agosti,2023 jumla ya Miradi ya maendeleo 07 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imemulikwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023.


Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mwenge wa uhuru utakimbizwa kilomita 167 katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukagua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali.


''Miradi itakayotembelewa ni pamoja na Barabara ya lami km1.25 katika Kata Bwanjai yenye thamani ya shilingi Milioni 484.8, Mradi wa Maji wa Kata ya Kitobo wa RUWASA wenye thamani ya shilingi milioni 802.6, Kituo cha Afya cha St. Thereza -Kajunguti wenye thamani ya shilingi milioni 96.0 ambapo kati ya hizo shilingi milioni 3.9 kutoka katika michango ya Mwenge na Wahisani milioni 92.1, Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira Katika Hospitali ya Wilaya ya Missenyi Kata ya Mushasha wenye thamani ya shilingi miloni 3.9, Mradi wa Ujenzi wa jengo la Abiria katika stendi ya Kyaka katika Kata ya Kyaka wenye thamani ya shilingi milioni 31.6, Mradi wa Vijana wa Kyaka Youth Construction and Technician katika kata ya Kyaka wenye thamani ya shilingi milioni 32 na Mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye Uhitaji Maalum pamoja na uzio katika Kata ya Kassambya katika Shule ya Msingi Bunazi na thamani ya mradi ni milioni 178.1 Alisema Kanali Sakulo.


Katika Mradi wa matengenezo ya barabara ya lami ya KAJAI-BWANJAI-BUYANGO yenye urefu wa kilomita 1.25 katika Kata Bwanjai yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 484.8, Ujenzi huu unajumuisha kusafisha eneo la kazi, kuchonga na kushindilia barabara, ujenzi wa kalavati 08 za duara, vivuko 12 vya miguu, uwekaji wa tabaka 03 za changarawe na kushindilia, lami, ujenzi wa mitaro pamoja na uwekaji wa alama za barabarani.

Mradi huu umesaidia kupitika kwa kipindi chote cha mwaka, kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii.Ujenzi huu ulianza 25 Agosti, 2021 na kukamilika 15 Januari, 2022 na umetekelezwa na mkandarasi PETER MULIMA wa Bukoba kupitia fedha za mfuko wa jimbo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.

Mradi wa Maji katika Kata ya Kitobo wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 802.6 uliopo katika Kata ya Kitobo katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. Mradi huu unahudumia wananchi 5,836 kutoka kaya 973 za vijiji vya Kitobo, Kijunja, Kashasha na Kyazi.

Mradi huu unajumuisha tenki la maji lenye ujazo wa lita 135,000, tenki dogo lenye ujazo wa lita 50,000, vituo 10 vya kuchotea Maji, Nyumba ya Mtambo 01, ulazaji wa Mabomba kwa 27.1km, Ujenzi wa ofisi 01, Ufungaji wa Tranfoma ya KVA 50 na Pampu 01 ya kusukuma maji. Mpaka sasa jumla ya kaya 102 na taasisi 07 zimeunganishiwa huduma ya maji na mradi umetatua changamoto ya kutumia muda mwingi na kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Mradi huu ulianza kujengwa tarehe 18/01/2022 na kukamilika 30/06/2023 na mkandarasi aitwaye LUTHER ENGENERING CO.LTD wa Mwanza kupitia fedha za Serikali Kuu.

Mradi wa Wodi ya Wagonjwa yenye thamani ya shilingi milioni 96 katika kituo cha Afya cha St. Therese - Kajunguti ambapo Michango ya Mwenge wa Uhuru ni shilingi milioni 3.9 na wahisani milioni 92.1.Ujenzi wa mradi huu ulianza mnamo 01/07/2022 na kukamilika 30/07/2023.

Mradi wa Uhifadhi Mazingira katika Hospitali ya Wilaya ya Missenyi iliopo katika Kijiji cha Bulembo katika Kata ya Mushasha wenye thamani ya shilingi milioni 3.9. Eneo hili limeandaliwa kwa ajili ya kuoandwa miti 8,000 ingawa mpaka sasa imepandwa miti 5,724 ikiwemo miti aina ya Paini na Miti ya Matunda kama vile Miembe na Miparachichi

Gharama za mradi huu ni kwa ajili ya ununuzi wa miche, maandalizi ya eneo, upandaji, umwagiliaji na usimamizi wa mradi, Lengo la mradi huu ni kwa ajili ya kutunza na kuhifadhi mazingira kama kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023 isemavyo "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa.

Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Abiria katika Stendi ya Mabasi Kyaka liliopo katika Kata ya Kyaka wenye thamani ya shilingi milioni 31. 6, Ujenzi huu umetokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri na ulianza kutekelezwa mnamo mwezi Septemba 2022 na kukamilika 03/03/2023 kwa lengo la kusaidia kuwakinga idadi ya watu 83 hadi 92 na mvua na jua wakati wa kusubiria usafiri au waanyabiashara wadogowadogo ndani ya stendi.

Mradi wa Vijana wa Kyaka Youth Construction and Technician (KYCT) kilichopo katika Kata ya Kyaka wenye thamani ya shilingi milioni 32. Kikunndi hiki kinajishughulisha na kufanya kazi za ufundi wa umeme kama vile kuweka miundombinu ya umeme kwenye nyumba binafsi na taasisi mbalimbali, kujenga njia za umeme vijijini na mjini , kutoa huduma ya usafiri wa pikipiki, magari, bajaji pamoja na uungaji wa vyuma(Kuchomelea).Kikundi kilianzishwa tarehe 06/09/2022 kikiwa na Mtaji wa shilingi Milioni 22 na baadae kilipata mkopo wa 04% kwa vijana utokanao na mapato ya ndani ya Halmashauri na kikundi.

Mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye Mahitaji maalum pamoja na uzio katika Shule ya Msingi Bunazi iliopo katika Kata ya Kassambya wenye thamani ya shilingi milioni 178.1, Gharama za ujenzi huu zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ni shilingi milioni 47, serikali kuu shilingi milioni 130 na jamii shilingi milioni1.1.Lengo la mradi ni kulaza wanafunzi wa kike 80 wenye mahitaji maalum ambao ulemavu wao hauwawezeshi kuhudhuria masomo kwa kwenda shuleni na kurudi nyumbani kila siku.

Ikumbukwe kwamba Mwenge wa uhuru 2023 utakesha katika eneo la uwanja wa Mashujaa na kwenda kukabidhiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa 12 Agosti, 2023.



Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa