• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Uviko19
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU

Posted on: December 9th, 2022

Leo tarehe 09 Disemba 2022 Wilaya ya Missenyi tumehitimisha maadhimisha ya sherehe za miaka 61 ya uhuru ambapo maadhimisho haya yalianza tangu tarehe 01 Disemba 2022 kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile usafi , kupanda miti , mashindano ya insha na kufikia kilele siku ya leo 09 Disemba 2022 ambapo kulikua na Mdahalo uliofanyika kama sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu hii muhumu kwa Taifa letu.

Katika maadhimisho haya mgeni rasmi alikua Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Wilson Sakulo na  hatimaye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Toba Nguvila aliwasili kujiunga na Wilaya ya Missenyi kwa ajili ya kuadhimisha kwa Pamoja maadhimisho haya yenye kauli mbiu ya MIAKA 61 YA UHURU ‘’AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU” na Mdahalo ulijikita kujadili MAENDELEO TULIOYAPATA BAADA YA MIAKA 61 YA UHURU.

‘’Moja ya matunda ya uhuru kwa sasa unatoka Mutukula hadi Dar es salaam ni lami tupu na una uwezo wa kuchagua barabara katika maeneo mbalimbali upitie barabara ya Biharamulo au upite Chato uchaguzi huu haukuwepo kipindi cha kabla ya uhuru.” Alisema Bw. Nguvila

Aidha kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ailiangazia Katika maeneo yaliyotia fora kwa kuendelea Zaidi ambayo ni Pamoja na sekta ya elimu haswa kutokana na ujenzi wa miundo mbinu mipya kama vile madarasa ambayo yameleta ufanisi mkubwa sana katika shule za msingi na sekondari.

‘’Upande  afya kutokana na ujenzi wa Hospitali Mpya ya Wilaya ambayo mpaka sasa imegharimu shilingi bilioni 1.3 zahanati zipo 30 ambapo awali zilikua 20 na vituo vipya vya afya 02 ambavyo ni Kanyigo na Kakunyu na vyote hivi vipo hatua za mwisho za umaliziaji’’. Alisema Sakulo.

Aliongeza kwa kusema Ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kutoka blioni 1.1 mwaka 2015/16 hadi kufikia bilioni 4.9 ambayo ni sawa na asilimia 135 kwa mwaka 2021/22.

Katika kuondoa adha katika barabara halmashauri ya Wilaya ya Missenyi  urefu wa barabara  umefikia kilomita  921 zinazohudumiwa.

Katika juma hili la maaddhimisho ya uhuru jumla ya miche ya miti 624 ikiwemo ya matunda, vivuli na miti ya mbao ilioteshwa katika eneo la hospitali mpya ya Wilaya ya Missenyi Pamoja na kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kuweka kumbukumbu katika kuadhimisha miaka 61 ya uhuru wa Tanzania bara.

Mdahalo wa leo uliweza kuhudhuriwa na wanafunzi 03 kutoka shule za msingi na 03 kutoka shule za sekondari ambao waliibuka washindi wa Insha na kukabidhiwa zawadi za vyeti kwa ajili ya shukrani ya ushiriki wao kutoka kwa mgeni rasmi, aidha walishsiriki wazee maarufu, wananchi na watumishi katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi.


Tarifa Kwa Umma

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera Region August 19, 2022
  • TAHADHARI YA EBOLA October 02, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA SEKONDARI October 05, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI TAREHE 08/11/2022. November 03, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.3 KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2022/23ROBO YA

    January 20, 2023
  • MRADI MPYA WA BOOST KUJENGA VYUMBA 12,000 VYA MADARASA

    December 22, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU

    December 09, 2022
  • MISSENYI DC: UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA UMEFIKIA ASILIMIA 98%

    November 27, 2022
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • JINSI YA KUOMBA MKOPO KUTOKA BODI YA MKOPO
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa