• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YAWAFIKIA WANANCHI WILAYANI MISSENYI

Posted on: April 15th, 2025

Leo Aprili 15, 2025 Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeanza katika Wilaya ya Missenyi ambapo wananchi wamejitokeza katika viwanja vya Igayaza Kata ya Nsunga na kuwasilisha kero zao kwa Wataalamu wa sheria.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nsunga, Wilayani Missenyi mapema leo Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amewataka wananchi kuwasema wale wote wanaofanya uhalifu, ukiukaji wa sheria, dhuruma na ukatili wa kijinsia ili wachukuliwe hatua.

"Ndugu zangu pale kwenye uhalifu na ukiukaji wa sheria muda wa kusema ni sasa, wale ambao wanafanya ukatili wa kijinsia na wale ambao wanadhurumu wajane na wanyonge muda wakusema ni sasa ili washughulikiwe". Amesema Dkt. Dumbaro.

Aidha, ameongezea kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kupitia Afisa Dawati na Mratibu wa Kampeni ya Huduma za Kisheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ili kusikiliza kero na changamoto za Kisheria zinazowakabili wananchi hata baada ya siku tisa zilizotengwa katika Wilaya ya Missenyi kuisha.

Pia amesisitiza kuwa kupitia msaada wa Kisheria haki, usawa na amani katika jamii vitapatikana hivyo kuwa chachu ya maendeleo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Florent Kyombo amesema kuwa uwepo wa Kampeni hii ni fursa kwa wananchi Wilayani Missenyi kutatua changamoto zao zinazowakabili, kwani baadhi ya wananchi kesi zao zimeshindwa kuendelea kutokana na kushindwa kumudu gharama za kuwalipa Mawakili.

Kwa upande wao wananchi waliojitikeza katika Viwanja vya Igayaza, Kata ya Nsunga Wilayani Missenyi wameipongeza Serikali kwa kuleta huduma za Kisheria karibu na maeneo yao, wakisema hatua hiyo itasaidia kutatua changamoto zao zinazohitaji msaada wa Kisheria.

Kampeni hii ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imezinduliwa rasmi Mkoani Kagera Aprili 14, 2025 ambapo kwa Wilaya ya Missenyi imeanza rasmi leo Aprili 15.

Kampeni hiyo yenye Kauli mbiu isemayo "Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo" imelenga kuwafikia wananchi walioko pembezoni kwa kuwawezesha kupata haki zao kwa njia ya sheria.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA MISSENYI

    May 16, 2025
  • WATENDAJI KATA NA VIJIJI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTOA ELIMU YA LISHE KWA JAMII

    May 14, 2025
  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa