• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

JIMBO LA NKENGE KUBADILISHWA JINA KUWA JIMBO LA MISSENYI

Posted on: March 11th, 2025

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Missenyi (DCC) leo Machi 11, 2025 imejadili na kupitisha mapendekezo ya kubadili jina la Jimbo la uchaguzi kutoka Jimbo la Nkenge na kuitwa Jimbo la Missenyi.

Akimkaribisha Mwenyekiti wa Kikao ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga kufungua kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bi. Tapita Tuvana amesema kwamba lengo la kikao hicho ni kuhakikisha Kamati ya Ushauri ya Wilaya inajadili pendekezo la kubadili jina la Jimbo la uchaguzi ili baada ya hapo kuwe na msimamo mmoja kama Wilaya.

Akiwasilisha taarifa ya mapendekezo ya kubadili jina la Jimbo la uchaguzi kutoka Jimbo la Nkenge na kuitwa Jimbo la Missenyi kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bi. Catherine Peter amesema kwamba mnamo tarehe 26/02/2025 Tume huru ya Uchaguzi ya Taifa ilitoa tangazo kwa umma pamoja na barua ya maelezo ikihusu kuanza kwa mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi Tanzania bara.

Kutokana na taarifa hiyo, tangazo liliwasilishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa tarehe 28/02/2025 ambapo Baraza lilichambua na kupendekeza kuwa jina la jimbo libadilike kutoka Jimbo la Nkenge na kuitwa Jimbo la Missenyi na hii ni kutokana na sababu mbalimbali.

Moja ya sababu hizi ni kutokuwepo kwa mfanano wa jina la Wilaya na Jimbo la uchaguzi hivyo kupelekea jina la Nkenge kutofahamika sana na kutotumika katika nyaraka mbalimbali za kimawasiliano baina ya serikali, chama na utendaji kazi wa kila siku.

Pili, jina Nkenge kutumika kwenye Tume huru ya Uchaguzi na uwakilishi wa Mbunge Bungeni hivyo kupelekea jina hili kutumika na muhimili mmoja wa dola ambao ni Bunge na kuacha mihimili mingine ikiwemo Mahakama na Serikali.

Aidha, Wajumbe wa Kamati wamepata nafasi ya kujadili na hatimaye kwa kauli moja wameridhia kupitisha jina la Missenyi kuwa jina la Jimbo la Uchaguzi na kuanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.

Mwenyekiti wa Kikao ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amehitimisha kikao hicho kwa kuwashukuru Wajumbe wote kwa ushiriki wao na kuwataka kuendelea kushirikiana na kuacha chuki na majungu.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia Vijiji, Kata, Halmashauri na ngazi ya wilaya ikiwa ni pamoja viongozi wawakilishi wa vyama vya siasa na madhebu ya dini mbalimbali.

Tarifa Kwa Umma

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA WATENDAJI WA UCHAGUZI NGAZI YA VITUO October 22, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WA KARANI, WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA JIMBO LA MISSENYI October 10, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BILIONI 3.4 ZA RAIS SAMIA KUTATUA CHANGAMOTO YA HUDUMA ZA AFYA WILYA YA MISSENYI

    October 16, 2025
  • WAZEE WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUDUMISHA AMANI NA KUHIMIZA MALEZI BORA KWA VIJANA

    October 01, 2025
  • HALMASHAURI YAWAKUTANISHA WADAIU WA KILIMO NA TAASISI ZA KIFEDHA

    September 24, 2025
  • WAKAZI 7,562 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MUTUKULA

    September 10, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa