• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

CHANGAMOTO ZA WAKULIMA WA MIWA MISSENYI ZAPATA UFUMBUZI

Posted on: September 13th, 2024

Leo Septemba 13, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Missenyi  Mhe. Kanali (Mst) Hamis Maiga amefanya kikao na Uongozi wa Kiwanda cha Kagera Sugar na wawakilishi wa vyama vya ushirika vya wakulima wa Miwa katika Wilaya ya Missenyi kwa lengo la kutatua changamoto zinazo wakabili  Wakulima hao.


Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mhe.Kanali (Mst) Hamis Maiga amewasihi wakulima wa miwa na kiwanda cha Kagera Sugar kupendana kwasababu wanategemeana.



"Wakulima wa miwa na Kagera Sugar maisha yenu yanategemeana, watu wanaotegemeana lazima wapendane mkipendana mtakuwa wamoja na hizi changamoto zilizopo itakuwa rahisi kuziondosha, kwahiyo nina imani suluhu itapatikana katika kikao hiki".


Aidha changamoto ambazo zimepatiwa ufumbuzi na kufikiwa makubaliano katika kikao hicho ni pamoja na; wakulima waendelee na utaratibu wa kuwa na wakataji wao na Kiwanda kitatoa wakataji 200 kwa kuanzia, AMCOS kupeleka tani 1,200 kwa siku sawa na tani 36,000 kwa mwezi, malipo ya Wakandarasi watalipwa baada ya siku 14 na malipo ya wakulima yatalipwa baada ya siku 60, kuhusu upimaji wa ubora wa miwa utafanyika kwa miwa ya ajali ya moto na mkulima atashirikishwa kwenda kuona namna wanavyopima na mwisho majibu yatatolewa kwa AMCOS kwa njia ya maandishi, kiwanda kitachukua miwa yote ya wakulima lakini wakulima wajitahidi miwa ifike ndani ya masaa 24 hadi 36, aidha, Kikao kimeadhimia kwamba ajali za moto zipimwe kisha  mkulima na viongozi wa AMCOS washirikishwe kuchukua miwa ili miwa iweze kufika kiwandani, na kuhusu mabadiliko ya mbegu mpya wakulima wapewe muda wa kumaliza mbegu ya zamani na elimu itolewe  kabla ya kuanza kulima mbegu mpya yenye matokeo mazuri na tija katika uzalishaji wa sukari.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mhe. Projestus Tegamaisho amevitaka vyama vya ushirika kutafuta wataalamu wa uchumi na wanasheria ili wawafundishe na kuwasaidia wakulima wa miwa katika kusaini mikataba na namna bora ya kupata faida.


Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mhe Projestus Tegamaisho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. John Paul Wanga, Uongozi wa Kiwanda cha Kagera Sugar ukiwakilishwa na Bw. Sanjeev Mishra ambaye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho na Viongozi mbalimbali wa Wilaya na vyama vya ushirika.



Tarifa Kwa Umma

  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2025 March 06, 2025
  • TANGAZO LA UTOAJI WA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO WILAYANI MISSENYI March 03, 2025
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025 February 24, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WALIOKOSA MIKOPO KWA AWAMU YA KWANZA WAPEWE ELIMU

    April 30, 2025
  • WANANCHI MISSENYI WAASWA KUENZI MUUNGANO KWA VITENDO

    April 26, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAJIRIDHISHA NA UTARATIBU WAKUBADILI JINA LA JIMBO LA UCHAGUZI NKENGE

    April 25, 2025
  • 60% YA MAPATO YA NDANI INAPELEKWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

    April 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HALMASHURI YATOA VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WALEMAVU
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa