• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni na Vitengo
      • Divisheni
        • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
        • Divisheni ya Elimu Sekondari
        • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo Vijijini na Mjini
        • Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu
        • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
        • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
        • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Vitengo
        • Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo
        • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Huduma za Kisheria
        • Kitengo cha TEHAMA
        • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Kitengo cha Huduma za Manunuzi
        • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
    • Tarafa
      • Tarafa ya Missenyi
        • Kata ya Mutukula
        • Kata ya Minziro
        • Kata ya Nsunga
        • Kata ya Kakunyu
        • Kata ya Kassambya
        • Kata ya Kyaka
        • Kata ya Mushasha
        • Kata ya Kilimilile
        • Kata ya Mabale
        • Kata ya Bugorora
      • Tarafa ya Kiziba
        • Kata ya Bugandika
        • Kata ya Kitobo
        • Kata ya Buyango
        • Kata ya Ruzinga
        • Kata ya Bwanjai
        • Kata ya Gera
        • Kata ya Ishozi
        • Kata ya Ishunju
        • Kata ya Kanyigo
        • Kata ya Kashenye
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha

BARAZA LA MADIWANI LAIDHINISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 51.1 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/26

Posted on: January 28th, 2025

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi leo tarehe 28 Januari 2025 limeanza Mkutano Maalum wa siku mbili kwa ajili ya kujadili na kuidhinisha Mpango wa maendeleo na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2025/2026.

Katika Mkutano huo jumla ya shilingi Bilioni 51.1 zimeidhimishwa kwa ajili ya Mpango wa maendeleo na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 ikiwa ni ongezeko la bilioni 9.5 sawa na asilimia 22.8 ya Mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ilikua shilingi bilioni 41.6.

Akiwasilisha taarifa ya Mapitio Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. John Paul Wanga alisema, katika kufanya Mapitio ya mapato ya ndani kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, kwa mwaka wa fedha 2023/24 Halmashauri iliakisia kukusanya shilingi bilioni 5.3 na ikakusanya shilingi bilioni 8.2 sawa na aslimia 154 na mwaka huu wa fedha unaondelea 2024/25 maakisio yalikua bilioni 6.9 na mpaka kufikia nusu mwaka yaani Desemba 2024 makusanyo yalifikia bilioni 5.2 sawa na asilimia 76 na kwa mwaka ujao wa fedha 2025/26 maakisio ni shilingi bilioni 9.06 sawa na ongezeko la shilingi bilioni 2.1 sawa asilimia 23.

Kwa upande wake Mheshimiwa Projestus Tegamaisho ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri alibainisha miradi ya kimkakati ambayo inatarajiwa kuongeza mapato ya Halmashauri katika Mwaka wa fedha 2025/26 ambayo ni pamoja na Mradi soko la ndizi linalo ambatana na Gulio katika kata ya Gera, Kufungua eneo la Sabasaba katika Kata Bugandika kwa ajili ya Soko maalum la ndizi aina ya Fia na kufanya shughuli za sabasaba na maadhimisho ya wiki ya Missenyi.

Mhe. Tegamaisho alisisitiza kwamba katika Kata ya Kakunyu kutafanyika uthamini na kulipa fidia ili kupanua eneo la mnada wa Lyabatura sambamba na kufungua Mnada wa Mbuzi na Gulio katika kijiji cha Bugango ambapo mkandarasi amepatikana na ataanza kazi mara moja.

"Katika Kata ya Mutukula tunataka kuweka shughuli za uchakataji wa mazao katika eneo la Kabakesa na Kujenga Mutukula Complex Park hivyo tutafanya upembuzi yakinifu ili kujua mahitaji halisi ya maeneo hayo" Alisema Mhe. Tegamaisho.

Hata hivyo aliongezea kwamba katika Kata ya Kashenye kutawekwa Mtambo wa kuzalisha Barafu katika Mwalo wa Kabindi, kuimarisha uzio wa Mwalo na kupanga eneo la Kabindi ili wajenge katika mipango miji.

"Katika Kata ya Kassambya ujenzi wa Soko la Bunazi umetengewa shilingi bilioni 1.7 na soko likikamilika litakalogharimu takribani shilingi bilioni 5 ambapo mpaka sasa tuna shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi mwezi Machi 2025" Alisema Tegamaisho.

Alisisitiza kwamba katika maeneo ya Kata za Kassambya, Kyaka na Mutukula tumetenga fedha kwa ajili ya mpango Kabambe wa uendelezaji miji hio ili kuandaa maeneo hayo kuwa miji.

Maandalizi ya Uandaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 umezingatia ilani ya Uchaguzi ya Mwaka wa fedha 2020/2025 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwongozo wa Mpango na bajeti 2025/2026, Vipaumbele vya Halmashauri vilivyoibuliwa na wananchi, Mpango mkakati wa Halmashauri 2020/25, Maelekezo ya viongozi wa ngazi ya Kitaifa na Mkoa, Sera za Kisekta, Dira ya Maendeleo ya Taifa2025, Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015, Malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG's), Agenda ya uboreshaji wa kilimo 10/30 na Mpango wa Kuandaa kesho ya vijana kupitia BBT.

Tarifa Kwa Umma

  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MISSENYI KUWAAGIZA WANAFUNZI VYUMA CHAKAVU June 03, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAPOKEZI YA SHILINGI MILIONI 445 MWEZI MEI KUTOKA SERIKALI KUU May 13, 2025
  • JIMBO LA NKENGE LIMEFANIKIWA KUBADILISHWA JINA RASMI NA KUWA JIMBO LA MISSENYI. May 12, 2025
  • TANGAZO LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MISSENYI April 14, 2025
  • Tazama zote

Habari mpya

  • NGO's ZAASWA KUTOKUKUBALIANA NA MASHARTI MAGUMU YA WAFADHILI

    June 26, 2025
  • MISSENYI YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI SOKO LA KISASA BUNAZI

    June 20, 2025
  • MISSENYI YAPATA HATI SAFI MIAKA 10 MFULULIZO

    June 17, 2025
  • PONGEZI NA TUZO ZATOLEWA KWA WALIMU, SHULE NA KATA KWA UFAULU MWAKA 2024

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Video

TUMEPATA HATI SAFI, TUJIPONGEZE
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    Sanduku la Posta: 38 Kyaka - MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: +255 28 298 2836

    Namba ya simu : +255 28 298 2836

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa